"Chupa moja ya maji ilinigharimu Sh1,500" Vera azungumzia gharama kali ya sherehe ya kufichua jinsia

Amesema kuwa maji ambayo wageni waliohudhuria walikunywa hayapatikani hata kwa maduka makubwa.

Muhtasari

•Mwanasoshalaiti Vera Sidika amefichua kuwa ilimgharimu shilingi 105, 000 kununua chupa 70 za maji ya kuburudisha wageni kwenye hafla ya kufichua jinsia ya mtoto anayetarajia.

•Alisema kuwa chupa moja ya maji ilimgharimu shilingi 1,500, takriban mara hamsini zaidi ya bei ya kawaida ya chupa maji nchini Kenya.

Image: INSTAGRAM//VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amefichua kuwa ilimgharimu shilingi 105, 000 kununua chupa 70 za maji ya kuburudisha wageni kwenye hafla ya kufichua jinsia ya mtoto anayetarajia.

Vera ambaye alifanya sherehe ghali mno usiku wa Jumamosi amesema kuwa maji ambayo wageni waliohudhuria  walikunywa hayapatikani hata kwa maduka makubwa.

Alisema kuwa chupa moja ya maji ilimgharimu shilingi 1,500, takriban mara hamsini zaidi ya bei ya kawaida ya chupa maji nchini Kenya.

Kwa kawaida chupa ya maji ni kati ya shilingi 20-40 nchini.

"Maji pekee yake ilinigharimu shilingi 105,000, chupa moja shilingi 1, 500. Maji ambayo hayawezi patikana kwa maduka makubwa. Lazima uagize kwa tovuti" Vera alisema.

Vera pia alikanusha madai kuwa alikataa kumlipa mcheshi Akuku Danger ambaye alimkodisha vifaa vya sauti.

Akuku Danger alikuwa amedai kuwa mwanasoshalaiti huyo alikosa kumlipa baki ya shilingi elfu  tano baada ya kufikisha vifaa hivyo kwenye sherehe.

Vera alisema kuwa huwa analipia huduma na bidhaa zote kabla ya kuzipokea