Jinsia ya mtoto wa Vera Sidika hatimaye yafichuliwa

Muhtasari
  • Jinsia ya mtoto wa Vera Sidika hatimaye yafichuliwa
  • Mjasiriamali  na mwanasosholaiti Vera Sidika  mwenye ujauzito anastahili kujifungua baada ya miezi mitatu
  • Vera mpenzi wake Brown Mauzo wanatarajia mtoto wao wa kwanza au kifungua mimba wao
Vera Sidika akifichua mimba
Vera Sidika akifichua mimba
Image: Instagram

Mjasiriamali  na mwanasosholaiti Vera Sidika  mwenye ujauzito anastahili kujifungua baada ya miezi mitatu.

Vera mpenzi wake Brown Mauzo wanatarajia mtoto wao wa kwanza au kifungua mimba wao.

Vera, ambaye anafurahi sana kukaribisha kifurushi chake cha furaha, alifanya sherehe nzuri ya kufichua jinsia Jumamosi, Julai 10, jijini Nairobi.

Na baada yautni mwingi kutoka kwa Vera, mwishowe ilifichuliwakuwa anatarajia mtoto msichana.

Hii inatimiza tu matakwa ya mumewe, Brown Mauzo ambaye alikuwa na matumaini kuwa watapata mtoto wa kike.

Brown Mauzo lazima afurahi sana juu ya habari ya jinsia ya mwanawe kwani alikuwa na matumaini.

Kabla ya siku ya sherehe, Vera Sidika hakuweza kuficha wasiwasi wake kwani alitamani kujua jinsia ya mtoto

Kulingana na mchekeshaji Eric Omondi, endapo wanandoa watapata kifunua mimba msichana walikuwa na mapenzi tele, ilhali wakimpata mvulana kweli walifanya tendo la ndoa, alimtania Vera Sidika.

Awali kwenye ukurasa wake wa instagram aliweka wazi kwamba alibeba ujauzito wake siku ya wapendanao mwaka huu.

Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia mwanasosholait huyo kila la heri.