'Kwa sasa nataka kufurahia maisha na familia' Vera Sidika aeleza sababu hakuwahi taka ujauzito

Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa aliacha kupanga uzazi mwezi wa Januari na akaweza kuwa mjamito katika jaribio lao la kwanza, jambo ambalo lilimshangaza sana.

Muhtasari

•Vera ambaye kwa sasa ana ujauzito wa wiki kumi na mbili ameeleza kwamba alikuwa akihisi hayuko tayari na aliishi kupanga uzazi kabla ya kufanya maamuzi ya kupata mtoto na mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki Brown Mauzo.

•Alisema kuwamba pamoja na mpenzi wake walikuwa wakitaka kufurahia ndoa yao kwanza kabla ya kuanzisha familia. Alisema kwamba walionelea kuwa huu ndio mwaka mzuri kupata mtoto. 

Vera Sidika na Brown Mauzo
Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti mashuhuri Vera Sidika amezungumzia  safari ya ujauzito wake na akataja sababu kwa nini hakutaka kupata mtoto hapo awali.

Vera ambaye kwa sasa ana ujauzito wa wiki kumi na mbili ameeleza kwamba alikuwa akihisi hayuko tayari na aliishi kupanga uzazi kabla ya kufanya maamuzi ya kupata mtoto na mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki Brown Mauzo.

"Watu ambao wananifuata mitandaoni wanajua kwamba nimekuwa nikitumia dawa za kuzuia ujauzito.. Kweli napenda watoto lakini huwezi pata mtoto kwa sababu tu unataka kupata mtoto, ni sharti uwe tayari. Kama wanawake ni lazima tuwe tayari kisaikolojia kabla tuanze kupata watoto kwa sababu watoto wanakuja na majukumu mengi.

Huwezi pata mtoto leo kisha ukamrejesha kesho, huyo ni mtoto na yumo maishani mwako milele" Vera alisema kupitia mtandao wa YouTube.

"Ni lazima kwanza ningehakikisha kuwa niko na mpenzi mwema, ni lazima ningehakikisha niko tayari, nilitaka kuhakikisha kwamba naweza jikimu kifedha ili kuzuia kuwa na majuto. Nataka kumpa mtoto wangu malezi bora" Aliendelea kusema.

Vera ambaye ana umri wa miaka 31 alisema kuwa alitaka kufurahia maisha ya ujana kwanza  kwani hakuwa tayari na kwa kuwa sasa amezuru mahali kwingi duniani angetaka kufurahia maisha  pamoja na familia.

" Kwangu nilichukua muda wangu kwani sikuwa tayari, nilikuwa naishi maisha ya msichana mdogo. Nimezuru kila mahali; nimeenda Paris, Marekani, Uingereza, kila mahali pataje. Nimekuwa pale, nimefanya. Kwa sasa nataka kupata hisia hizo pamoja na familia. Ni gani gani kuenda likizo na familia? Inapendeza, sio?" Alisema Vera.

Alisema kuwamba pamoja na mpenzi wake walikuwa wakitaka kufurahia ndoa yao kwanza kabla ya kuanzisha familia. Alisema kwamba walionelea kuwa huu ndio mwaka mzuri kupata mtoto. 

Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa aliacha kupanga uzazi mwezi wa Januari na akaweza kuwa mjamito katika jaribio lao la kwanza, jambo ambalo lilimshangaza sana.

Vera amewashauri wanawake kusubiri hadi wakati watahisi kuwa wako tayari ndio wapate watoto.