logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wacheshi Jalang'o, Otoyo na Njoro wajitolea kulipa karo ya binti wa marehemu Papa Shirandula

achozi ya furaha yalimtiririka mjane wa  marehemu Charles Bukeko almaarufu kama Papa Shirandula  baada ya mtangazaji Jalang'o kutangaza kuwa angechukua jukumu la kuelimisha binti yake mdogo kwa jina Sherry

image
na Radio Jambo

Habari19 July 2021 - 02:44

Muhtasari


•Kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka moja tangu kuaga kwa mwigizaji na mcheshi tajika  Papa Shirandula ambayo ilifanyika Jumapili, Jalang'o aliahidi kuwa angegharamia karo yote ya Sherry hadi chuo kikuu kwa ushirikiano na wacheshi wenzake Captain Otoyo na Njoro.

•Bukeko aliaga mnamo Julai  18 alipokuwa anakimbizwa hospitali kutokana na matatizo ya kupumua.

Machozi ya furaha yalimtiririka mjane wa  marehemu Charles Bukeko almaarufu kama Papa Shirandula  baada ya mtangazaji Jalang'o kutangaza kuwa angechukua jukumu la kuelimisha binti yake mdogo kwa jina Sherry. 

Wakiwa kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka moja tangu kuaga kwa mwigizaji na mcheshi tajika  Papa Shirandula ambayo ilifanyika Jumapili, Jalang'o aliahidi kuwa angegharamia karo yote ya Sherry hadi chuo kikuu kwa ushirikiano na wacheshi wenzake Captain Otoyo na Njoro.

"Sisi watatu; Jala, Otoyo na Njoro tunataka kuchukua jukumu la kulipa karo yote ya binti yangu hapa (Sherry). Kutoka leo mama usiwahi jali tena mambo ya karo. Tungetaka utuletee taarifa ya karo iwe leo, iwe kesho mimi mwenyewe nitakupatia cheki ya kutoka saa hii hadi amalize shule ya msingi na hata akiingia kidato cha kwanza mambo yake usiwahi jali. Kutokea leo Sherry ni wetu": Jalang'o alitangaza.

Njoro akimpanguza mjane wa Bukeko machozi

Mtangazaji huyo alisema kuwa alimtaka marehemu Papa afurahi kutoka mahali aliko kwani isingalikuwa ni yeye hawangekuwa hawangekuwa wamepata mafanikio ambayo wanayo kwa sasa.

Mjane wa Papa ambaye alikuwa amewezwa na hisia aliwashukuru kwa kitendo chao cha ukarimu.

"Nashukuru Mungu kwani yeye ni Mungu wa suluhu. Kile ambacho Jalang'o amefanya kimeyeyusha moyo wangu. Ni wiki moja tu niliwanga nafikiria kuhusu karo ya shule. Mungu ameleta suluhu. Asante." Mkewe Bukeko alisema

Watatu hao walijitolea kusaidia binti ya mtu ambaye aliwafungulia milango ya sanaa na kuwapa umaarufu mkubwa nchini kama ishara ya heshima.

Bukeko aliaga mnamo Julai  18 alipokuwa anakimbizwa hospitali kutokana na matatizo ya kupumua.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved