'Mola alinitumia bwana ambaye hajawahi onja pombe' Vera azungumzia jinsi Mauzo alimsaidia kusahau vileo

Mwanasoshalaiti huyo alieleza furaha yake kuona kuwa mtoto ambaye anatarajia atazaliwa kwa familia isiyo ya walevi.

Muhtasari

•Vera ambaye kwa sasa ana ujauzito wa takriban wiki kumi na nne amedai kuwa hatua yake kukaribisha  mpenziwe  Brown Mauzo maishani mwake mwezi Agosti mwaka uliopita ilimsaidia sana kusahau pombe kwaniyeye  hajawahi kuionja kamwe maishani.

•Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa ingawa yeye mwenyewe alikuwa mtumizi wa pombe hapo awali, hakuwa anakunywa sana. Amesema kuwa alikuwa akikunywa tu wakati anapiga sherehe.

Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti Vera Sidika anajivunia kumaliza miezi 15 bila kupiga maji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amekiri kuwa mara yake ya mwisho kutumia kileo ilikuwa mwezi Machi mwaka uliopita.

Vera ambaye kwa sasa ana ujauzito wa takriban wiki kumi na nne amedai kuwa hatua yake kukaribisha  mpenziwe  Brown Mauzo maishani mwake mwezi Agosti mwaka uliopita ilimsaidia sana kusahau pombe kwaniyeye  hajawahi kuionja kamwe maishani.

Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa ingawa yeye mwenyewe alikuwa mtumizi wa pombe hapo awali, hakuwa anakunywa sana. Amesema kuwa alikuwa akikunywa tu wakati anapiga sherehe.

"Mara ya mwisho nilikunywa pombe ni Machi 2020. Yup! Sikuwa nakunywa sana lakinI. Mimi hukunywa hadharani wakati tu napiga sherehe. Tangu Corona ije mwaka uliopita sijakuwa nikienda klabu  kwa hivyo hakuna pombe nilikunywa.

Halafu bwanangu akaja mwezi Agosti, Mungu alinitumia bwana ambaye hajawahi kuonja pombe maishani mwake. Jambo hilo lilifanya kusahau pombe kuwa rahisi .  

Ni mwaka mmoja unusu umetamatika saa. Wow! niliacha kukunywa hata kabla nipate ujauzito" Vera alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alieleza furaha yake kuona kuwa mtoto ambaye anatarajia atazaliwa kwa familia isiyo ya walevi.

"Kusema kweli najivunia sana kuona kuwa mtoto wetu atazaliwa kwa familia ambayo haitukii pombe. Mama sober na baba sober. Mungu ni mwema." Alisema Vera.

Wiki moja iliyopita Vera alifichua kuwa amebeba mtoto wa kike. Alisema kuwa anatarajia kuwa amejifungua  kufikia mwezi Desemba mwaka huu.