Mhubiri David Muriithi ashtakiwa kwa madai ya kutelekeza mtoto, Mwanamke ataka kulipwa 100,000 kila mwezi

Mwanamke huyo anadai kuwa alipatana na mhubiri huyo mwaka wa 2018 na kujitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi ambayo yalipelekea kuzaliwa kwa mtoto mvulana mwezi Januari mwaka wa 2018

Muhtasari

•Mwanamke huyo amemshtaki mtumishi huyo wa Mungu wa kanisa la House of Grace kwa madai ya kutelekeza majukumu yake katika ulezi wa mtoto anayedai kuwa wake.

•Kulingana na nyaraka za korti, Muriithi ametishia kutotoa usaidizi wowote kwenye ulezi wa mtoto huyo akidai kuwa yeye ni mhubiri aiyelipwa.

Mhubiri David Muriithi
Mhubiri David Muriithi
Image: FACEBOOK// HOUSE OF GRACE

Habari na Annette Wambulwa

Mwanamke mmoja anamtaka mhubiri mashuhuri David Muriithi kumpatia posho la shilingi 100,00 kila mwezi kugharamia mahitaji ya mtoto wa miaka miwili anayedai kupata naye.

Mwanamke huyo amemshtaki mtumishi huyo wa Mungu wa kanisa la House of Grace kwa madai ya kutelekeza majukumu yake katika ulezi wa mtoto anayedaiwa kuwa babake.

Anadai kuwa alipatana na mhubiri huyo mwaka wa 2018 na kujitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi ambayo yalipelekea kuzaliwa kwa mtoto mvulana mwezi Januari mwaka wa 2018.

Kupitia kwa wakili wake mwanamke huyo amedai kuwa Muriithi alifurahia sana kuskia habari kuhusiana na ujauzito huo na kufarahia hata zaidi wakati alijifungua.

"Mlalamishi anasema kuwa wakati wa ujauzito wake mshtakiwa alikuwa anamsaidia sana na alikuwa tayari kumwajibikia pamoja na mtoto wao" Omari alisema.

Hata hivyo Omari alisema kuwa mteja wake amkuwa akigharamia mahitaji ya mtoto huyo peke yake tangu kuzaliwa kwake.

Kulingana na nyaraka za korti, Muriithi ametishia kutotoa usaidizi wowote kwenye ulezi wa mtoto huyo akidai kuwa yeye ni mhubiri aiyelipwa.

Mlalamishi anasema kuwa Muriithi anamnyima mtoto wake haki yake kwa kukosa kugharamia mahitaji yake.

"Mlalamishi anasema kuwa Muriithi ni mhubiri katika kanisa inayotambulika sana nchini na ambaye anaishi maisha ya kifahari na hayuko  tayari kumpa mtoto wake maisha kama yale jambo ambalo linaashiria ubaguzi kwa upande wake" Wakili Omari alisema.

Omari alisema kuwa mtoto huyo alikuwa amehitimu umri wa kujiunga na shule na kwa hivyo mtumishi huyo wa Mungu anafaakumsaidia mama ya mtoto kulipa karo ya shule na mahitaji mengine.

Mwanamke huyo anadai kuwa Muriithi hataki kujihusisha kwa namna yoyote katika ulezi wa mtoto huyo licha yake kujua kuwa ndiye baba mzazi.

Omari alisema kuwa Muriithi ana jukumu la kulea mtoto huyo ambalo anafaa kulichukua na kuhakikisha kuwa mahitaji yake  yameshughulikiwa hadi atimie umri wa miaka 18.

Mlalamishi anasema kuwa karo ya shule ya Kiota ni Sh1,000 za saluni, Sh5000 za burudani,Sh 3,000, Sh2000 za vifaa vya kuchezea na Sh 3000 za huduma zingine

Mahakama imeagiza mwanamke huyo kumkabidhi Muriiithi wasilisho lake na kesi hiyo kuendelea mnamo Agosti 25.