"Niko single na sitafuti mpenzi" Zari Hassan adhihirisha kuwa hachumbiani na yeyote kwa sasa

Mapema mwezi uliopita Zari aliashiria dalili kuwa uhusiano wake na mpenzi wake wa hivi karibuni Dark Stallion ulikuwa umefika hatima.

Muhtasari

•Alipokuwa anajibu swali la shabiki wake mmoja aliyetaka kujua hali yake ya ndoa, mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa kwa sasa ako 'single' na hata hatafuti mchumba.

•Mwanasoshalaiti huyo kutoka Uganda ana watoto wawili pamoja na Diamond na wengine watatu kutoka ndoa yake ya kwanza na mume wake wa kwanza marehemu Ivan Semwanga ambaye alifariki mwaka wa 2017, miaka minne baada yao kutengana.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Aliyekuwa mke wa nyota wa bongo Diamond Platnumz, mfanyibiashara Zari Hassan amesisimua wanamitandao baada ya kutangaza wazi kuwa kwa sasa hana mchumba.

Alipokuwa anajibu swali la shabiki wake mmoja aliyetaka kujua hali yake ya ndoa, mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa kwa sasa ako 'single' na hata hatafuti mchumba.

"Mama Tee, pole kwa kuuliza lakini kwa sasa uko single ama umechukuliwa tayari?" Shabiki kwa jina @iamofficialanwar aliuliza

Mama huyo wa watoto watano hakusita kumjibu shabiki huyo na jibu lililoibua mdahalo mitandaoni.

"Niko single na sitafuti" Zari alisema.

Mapema mwezi uliopita Zari aliashiria dalili kuwa uhusiano wake na mpenzi wake wa hivi karibuni Dark Stallion ulikuwa umefika hatima.

Zari alifuta picha zote za Stallio kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuweka ujumbe wenye maana fiche  ambao uliibua dhana kuwa huenda walikuwa wametengana.

Ninampeza, lakini ilibidi nimuache aende. Ikiwa haijengi mimi sitaitunza,"   Zari aliandika.

Zari ambaye kwa sasa anaishi Afrika Kusini alitambulisha Dark Stallion kama mpenzi wake mwezi Februari mwakani baada ya kumficha hadharani kwa kipindi.

Mwanasoshalaiti huyo raia wa Uganda ana watoto wawili pamoja na Diamond na wengine watatu kutoka ndoa yake ya kwanza na mume wake wa kwanza marehemu Ivan Semwanga ambaye alifariki mwaka wa 2017, miaka minne baada yao kutengana.