'Ninampeza, lakini ilibidi nimuache aende,'Zari asema baada ya kufuta picha akiwa na mpenzi wake

Muhtasari
  • Zari afuta picha akiwa na mpenzi wake mitandaoni

Mfanyabiashara wa Uganda anayeishi Afrika Kusini Zari Hassan ameibua wasiwasi kati ya wafuasi wake milioni 9.3 baada ya kuweka ujumbe wa siri, ambao sasa umehusishwa na uhusiano wake mpya.

Zari amefuta picha zote alizowahi kupiga na mpenzi wake anayejulikana kama Dark Stallion, kitu ambacho kimewaacha mashabiki wengi wakiwa na wasiwasi.

Katika ujumbe wake wa siri, Zari alisisitiza kwamba ilimbidi amwache aende kwa sababu hawakusaidiana  kwa njia yoyote.

“Ninampeza, lakini ilibidi nimuache aende. Ikiwa haijengi mimi sitaitunza," Aliandika Zari.

Zari alifunua uso wa mpenzi wake mpya mnamo Februari 14, baada ya miezi ya kumuweka mbali na macho ya umma.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wanamitandao kumuona "Dark Stallion" kwani picha zote za awali alipigwa akiwa ameficha uso wake.

Kufunuliwa kulikuja siku ’baada ya kushambuliwa  na wakosoaji ambao walikuwa wakidai kuwa mapenzi na " Dark Stallion "hayatadumu.

Sosholaiti huyo alisema kuwa hajali ikiwa uhusiano huo utadumu au la, lakini alikuwa tayari na wakati mzuri na mpenzi wake mpya.