"Silali na baby daddies wangu" Akothee azungumzia uhusiano wake na 'baby daddies' pamoja na mpenzi wake

Akothee amedai kuwa yeye huchumbia mwanaume mmoja kwa wakati na uhusiano wao wa kimapenzi unapotamatika wanabaki maarafiki wa kawaida tu .

Muhtasari

•Mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee amewaonya wafuasi wake dhidi ya kuiga maisha yake haswa anavyohusiana na baba za watoto wake. 

•Akothee ameweka wazi kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na yeyote kati ya 'baby daddy' wake watatu na kudai kuwa mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks ndiye tu anayefurahia tunda lake kwa sasa.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee amewaonya wafuasi wake dhidi ya kuiga maisha yake haswa anavyohusiana na baba za watoto wake. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watano amedai kuwa yeye huchumbia mwanaume mmoja kwa wakati na uhusiano wao wa kimapenzi unapotamatika wanabaki maarafiki wa kawaida tu .

"Wacha niweke mambo wazi. Nachumbia mwanaume mmoja kwa wakati. Ikiisha tunabaki marafiki tukilea watoto. Uhusiano ambao tulijenga kwa kipindi cha miaka hiyo haujajengwa kwa msingi wa tendo la ndoa ama masuala ya kitandani. Watoto ambao tunao walitokana na mapenzi, ukiondoa tendo la ndoa kinachobaki ni urafiki, kuelewana na sote tunaelewa kuwa maisha lazima yasonge mbele." Akothee alisema.

Msanii huyo alikuwa akimjibu shabiki wake mmoja ambaye alifurahishwa na video iliyomuonyesha na watoto wake watatu wakiwa wameketi mezani wakifurahia chakula pamoja na mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks na  'baby daddy' wake mmoja mzungu.

"Naishi maisha safi, sina ghala la kuweka maisha yangu mengine. Unachokiona ndicho unapata, mimi sichezi na maisha haina reverse. Ni wakati wa chajio pamoja na familia" Akothee aliandika chini ya video hiyo.

Akothee ameweka wazi kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na yeyote kati ya 'baby daddy' wake watatu na kudai kuwa mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks ndiye tu anayefurahia tunda lake kwa sasa.

"Silali na 'baby daddies' wangu, nalala na mpenzi wangu. Baby daddies wako hapa kwa sababu ya watoto wetu, haya hayawezi kubadilika" Akothee alidai.