Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri nchini Vera Sidika amewakaripia marafiki wake waliokuwa wanamshawishi kuolewa na mzee tajiri hapo awali.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo mwenye umri wa miaka 31 amekiri kuwa kunao baadhi ya marafiki wake ambao walikuwa wanamshauri aolewe na mwanaume tajiri mwenye umri mkubwa ili aweze kujikimu kifedha.
Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa marafiki wale hawakutaka afurahie maisha jinsi anavyoyafurahia kwa sasa baada ya kufunga ndoa na mwanamuziki Brown Mauzo.
"Wengi wenu mlikuwa mnanishauri niolewe na mbaba kwa ajili ya pesa.. wanaume tajiri na wengineo blah blah blah. Kwa kwelihamkutaka nifurahie, nitosheke na nijihisi mkamilifu.
Je, huyo mbaba angenipa hata asilimi 1% ya mapenzi na kumakinika nami?? Angekuwa nami katika safari ya ujauzito wangu, anipende vizuri na anifanye nifurahie?? Hapanaa!!" Vera aliandika.
Amesema kuwa yeye hufuata roho yake na kamwe hasikilizi maneno ya watu.
Vera ameeleza kuridhika kwake baada ya kufunga ndoa na Mauzo na kudai kuwa mumewe anampenda sana bila masharti.
"Ndio maana huwa siskizi maneno ya watu. Huwa nafuata moyo wangu na kile ambacho unataka. Leo hii nina furaha kwa kweli. Nimeolewa na mwanaume anayenipenda bila masharti. Amekuwa nami kila sekunde, kila dakika, kila saa, kila siku, kila wiki, kila mwezi tangu niwe mjamzito. Amekuwa kando yangu kila wakati, mbaba wako hawezi" Amesema Vera.
Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa marafiki wale walimtaka awe kwenye ndoa iliyojaa masikitiko na asipate mapenzi wala furaha.
"Mlitaka niwe kwenye ndoa yenye masikitiko. Ningekuwa nashinda na dereva, walinzi na watumishi wengi wakinitunza wakati wa ujauzito wangu badala ya mbaba kwa sababu hata hana muda wangu. Kwa kweli hamkunitakia mazuri.
Sasa nyote mnanitumia jumbe mkisema Awww, uko na mume mzuri, naomba nami nipate kama huyo. Hahaa, nini kiliendelea kuhusu kupata mbaba?" Vera aliandika.
Vera kwa sasa amefunga pingu za maisha na mpenzi wake Brown Mauzo na wanatarajia mtoto wao wa kwanza baadae mwaka huu.