"Nimeumia kwa muda mrefu" Milly wa Jesus afunguka kuhusu tabia ya Kabi inayompa wasiwasi zaidi

Muhtasari

β€’Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Milly amefichua kuwa Kabi ana mazoea ya kulala akiwa amefungua macho, kitendo ambacho humtisha sana.

β€’Milly pia alieleza kwamba anahofia huenda mwanawe Taji akaiga tabia ya babake kwani pia yeye huwa hafungi macho kabisa anapolala.

Image: INSTAGRAM// KABI WA JESUS

Mwanavlogu Millicent Wambui almaruufu kama Milly wa Jesus amezungumzia tabia ya mumewe, Peter Kabi almaarufu kama Kabi wa Jesus ambayo humpa wasiwasi zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Milly amefichua kuwa Kabi ana mazoea ya kulala akiwa amefungua macho, kitendo ambacho humtisha sana.

Milly amesema kuwa jambo hilo limekuwa likimpa wasiwasi kwa kipindi cha miaka minne ambayo wamekuwa kwenye ndoa.

"Kusema kweli nimeumia kwa muda mrefu. Hebu tafakari miaka minne ya ndoa na haya ndiyo unaamkia kila asubuhi. @kabiwajesus aki tafadhali jifunze kufunga macho umenishtua ya kutosha. 

Kuweni na usiku mwema. Wacha mimi nijaribu kufunga mtu wangu macho" Milly aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Mashabiki wengi wamejumuika chini ya ujumbe huo kutoa hisia zao kuhusiana na suala hilo huku wengine wakimpa ushauri wa suluhu mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo. 

@kate_actress: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚pole babe , Aki nani Ako na therapist wa snoring 😭 nimeshokaaaa

@kabiwajesus: This photoshop thing will break marriages πŸ˜‚

@jackvike: πŸ˜‚πŸ˜‚ huwezi fanya Love hivi

@kymomusic: Selotape may be??πŸ˜‚

@tinnahke: Heri wako ni macho wangu mdomo na kumwaga mate.. nimekuvumilia sana

Tazama jumbe zaidi  za mashabiki chini ya ujumbe wa Milly:-

Mama huyo wa mtoto mmoja amesema kuwa walipokuwa wanafunga ndoa miaka minne iliyopita alidhani kuwa tabia ile ilikuwa inachangiwa na umri mdogo na alitumai kuwa ingekoma.

"Hayo ndiyo mambo napitia tangu tufunge ndoa, Mimi nilidhani kuwa tabia hiyo ingekoma. Nilidhani ni vile tu tulikuwa wadogo. Hebu tafakari kuchumbia mtu alafu uje kugundua baadae anavyolala. Lakini nashukuru nimepata suluhu" Alisema Millly.

Milly pia ameleza kwamba anahofia huenda mwanawe Taji akaiga tabia ya babake kwani pia yeye huwa hafungi macho kabisa anapolala.

Unajua hadi Taji, mi namuombea tu asifuate mkondo huo kwa sababu huwa analala akiwa amefungua macho. Natumai kuwa hatamuiga babake" Milly alisema.