"Mwanaume anapoona mwili wako hatumii akili kufikiria" Vera Sidika ashauri wanawake kumakinika wanaposhiriki tendo la ndoa

Muhtasari

•Mwanasoshalaiti huyo amewaonya wanawake dhidi ya kukubali kubeba ujauzito iwapo hawako tayari kulea wenyewe

•Vera amewaagiza wanawake wasikubali kufanya ngono bila kinga iwapo hawataki watoto kwa wakati ule kwani hakuna hakikisho iwapo mwanaume aliyehusika atakuwepo kwenye malezi

•Kulingana na Vera,  mwanaume ana uwezo wa kupachika wanawake wengi mimba kwa wakati mmoja na asonge mbele na maisha yake kana kwamba hakuna kitu kubwa alichofanya.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti mashuhuri  nchini Vera Sidika amesema kuwa wanaume huwa hawajalishwi na suala la ujauzito kwani wao hawana mfuko wa uzazi (Uterasi)

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanasoshalaiti huyo amewaonya wanawake dhidi ya kukubali kubeba ujauzito iwapo hawako tayari kulea wenyewe.

Kulingana na Vera,  mwanaume ana uwezo wa kupachika wanawake wengi mimba kwa wakati mmoja na asonge mbele na maisha yake kana kwamba hakuna kitu kubwa alichofanya. Kufuatia hayo, mfanyibiashara huyo  amewaagiza wanawake kuwa makini wasije wakajiingiza  kwenye mtego kwani mwanaume anaweza kusema chochote ilimradi tu apate anachotaka.

"Iwapo wanaume walikuwa na uterasi  najua vyema wangekuwa makini sana wasibebe ujauzito.. lakini kwa sababu hawajui ugumu wa ujauzito na kulea mtoto pekee yako, hawajali. Mwanaume mmoja anaweza kupachika wanawake 10 mimba kwa wakati mmoja na asonge mbele na maisha yake kama kwamba hakuna kitu kimefanyika.

Kwa hivyo wanawake kuweni makini kwa sababu wanaume hawa wanaweza kukwambia kila unachotaka kusikia wakati wanataka kitu. 'D' ni bure. Mwanaume anapoona makalio na sehemu zako za siri hatumii akili kufikiria" Vera amesema.

Mama huyo mtarajiwa amewashauri wanawake kumakinika zaidi wanapofanya maamuzi haswa wakati wa tendo la ndoa.

Vera amewaagiza wanawake wasikubali kufanya ngono bila kinga iwapo hawataki watoto kwa wakati ule kwani hakuna hakikisho iwapo mwanaume aliyehusika atakuwepo kwenye malezi.

"Mbona ukubali mfanye ngono bila kinga kama hutaki watoto. Mbona usitumie kondomu ya kike mwenyewe. Unapata ujauzito kwa sababu unataka. Huwezi pata tu ujauzito na kila mtu kwa sababu mmelala bila kinga. Sote tungekuwa na watoto 3-4 wa baba tofauti" Aliandika Vera.

Mwanasoshalaiti huyo amewashauri wanawake kujua wanachotaka maishani na kuwa tayari kisaikolojia, kifedha na kiakili kabla ya kufanya maamuzi yoyote.

Amesema kuwa kuna wanaume ambao ni wapenzi wazuri ila hawana uwezo wa kuwa baba wazuri kwa watoto wao

"Hebu jiulize, je uko na maisha ya usoni na jamaa huyo, je anaweza kuwa baba mzuri. Wanaume wengine ni wapenzi wazuri ila ni baba wabaya. Usikose kuwa mwangalifu kuona dalili" Vera ameshauri kina dada.

Amesema kuwa mwanaume anaposema kuwa hataki watoto huwa anamaanisha  maneno yake na kuwaarifu wanadada kuwa hakuna jinsi wanaweza kubadilisha hali ile.