"Wengine walitupatia miezi miwili" Vera Sidika awasuta waliodai kuwa ndoa yake na Mauzo haingedumu

Amesema kuwa walipojitokeza wengi hawakuamini kuwa ni kweli walikuwa wamefunga ndoa huku baadhi ya wanamitandao kwa wakati ule wakidai kuwa ilikuwa kiki.

Muhtasari

•Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa walichumbiana kisiri na mpenziwe kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kuweka uhusiano wao hadharani.

•Kulingana na mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31, kunao watu wengi ambao hawapendi kuona wengine wakifanikiwa kimahusiano, kibiashahara na kwa mambo mengine maishani.

•Wawili hao walijitosa kwenye ndoa mnamo Agosti 12 mwaka uliopita na mapenzi yao yameendelea kunoga huku sasa wakiwa safarini kuanzisha familia ndogo.

Image: INSTAGRAM//VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mjasiriamali mashuhuri Veronica Mung'asia almaarufu kama Vera Sidika amewasuta wale ambao hawakuamini kuwa ndoa yake na mwanamuziki Brown Mauzo ingedumu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa walichumbiana kisiri na mpenziwe kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kuweka uhusiano wao hadharani.

Amesema kuwa walipojitokeza wengi hawakuamini kuwa ni kweli walikuwa wamefunga ndoa huku baadhi ya wanamitandao kwa wakati ule wakidai kuwa ilikuwa kiki.

"Nakumbuka tukianza kuchumbiana tulikuwa tumejificha kisha tukatangaza hadharani miezi miwili baadae. Kila mtu alidai kuwa ni kiki" Vera alisema.

Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa kunao ambao walidai kuwa uhusiano wao haungedumu kwa zaidi ya miezi miwili huku wengine walisema kuwa yeye huwa na na mume tofauti kila anapoadhimisha siku ya kuzaliwa.

"Wengine walisema kuwa kila ninapoadhimisha siku ya kuzaliwa mimi huwa na mwanaume tofauti. Basi ninasherehekea siku ya kuzaliwa hivi karibuni. Wengine walitupatia miezi miwili na baada ya miezi miwili kuisha wakaongeza miezi mitatu. Ilifika hatua wakapoteza matumaini" Aliendelea kusema.

Kulingana na mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31, kunao watu wengi ambao hawapendi kuona wengine wakifanikiwa kimahusiano, kibiashahara na kwa mambo mengine maishani.

" Mimi husema, amini Mungu na kila kitu kitakuwa sawa kila wakati. Mungu anajua kuaibisha adui zako" Vera alisema.

Siku ya Alhamisi, Agosti 12 Vera na kipenzi chake Brown Mauzo waliadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao.

Wawili hao walijitosa kwenye ndoa mnamo Agosti 12 mwaka uliopita na mapenzi yao yameendelea kunoga huku sasa wakiwa safarini kuanzisha familia ndogo.

Siku chache zilizopita mwanasoshalaiti huyo alishangaza wanamitandao baada ya kukiri kuwa uhusiano wake wa sasa na mwanamuziki Brown Mauzo ndio mrefu zaidi kuwahi tokea maishani mwake. 

Vera Sidika alifichua kuwa kamwe hajawahi kuchumbia mwanaume mmoja kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja hapo awali.