"Nina bahati kuwa nawe kando yangu" Zari aandikiwa ujumbe maalum na mpenziwe akiadhimisha kufikisha miaka 41

Muhtasari

•Uhusiano kati ya wawili hao umeonekana kama kwamba ulizama tangu mwezi Julai wakati Zari alifuta picha za raia huyo wa Nigeria kwenye ukurasa wake wa Instagram.

•Siku ya Alhamisi @lyamzey_don alimwandikia Zari ujjumbe wa kipekee alipokuwa anasherehekea kufikisha miaka 41.

•'The Dark Stallion' alimtambulisha mama huyo wa watoto watano kama mkewe na kudai kwamba anajivunia sana kuhusiana naye.

Image: INSTAGRAM// LAMZEY DON

Huenda mwanasoshalaiti mashuhuri  kutoka Uganda Zari Hassan hajatengana kabisa lucky in na mpenzi wake 'The Dark Stallion' kama ilivyodhaniwa na wengi.

Uhusiano kati ya wawili hao umeonekana kama kwamba ulizama tangu mwezi Julai wakati Zari alifuta picha za raia huyo wa Nigeria kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, huenda bado mapenzi yamenoga kati yao kama chapisho la Stallion la hivi karibu kwenye mtandao wa Instagram linavyoashiria.

Siku ya Alhamisi @lyamzey_don alimwandikia Zari ujjumbe wa kipekee alipokuwa anasherehekea kufikisha miaka 41.

'The Dark Stallion' alimtambulisha mama huyo wa watoto watano kama mkewe na kudai kwamba anajivunia sana kuhusiana naye.

"Kheri za kuzaliwa kwa mwanamke anayeleta mwangaza maishani mwangu. Mpenzi wangu anayejali na mke nimpendaye. Wewe ndiye naweza ambia siri zangu na nina bahati sana kuwa nawe kando yangu. Kuwa na siku njema ambayo unastahili mke wangu mrembo. Kheri za kuzaliwa mama Pinto" Aliandika Stallion.

Miezi miwili iliyopita Zari matendo ya Zari kwenye mtandao wa Instagram yaliibua dhana kwamba kitumbua kilikuwa kimeingia mchanga na wawili hao walikuwa wamemua kukatiza uhusiano wao.

"Nampeza lakini ilibidi nimuache aende. Kama halinijengi basi sitaliweka" aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumza aliandika, ujumbe ambao ulionekana kuzungumzia Stallion.

Kabla ya hayo Zari alikuwa na mazoea ya kupakia picha zao kwenye ukurasa wake ila baada ya hapo hajaonekana tena akizipakia. The Stallion hata hivyo amepakia picha kadhaa baada ya hapo.