logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Suluhu ya maumivu na shida ni kifo.." Ujumbe wa Willy Paul waibua wasiwasi huenda amekabiliwa na msongo wa mawazo

Baba huyo wa watoto wawili amezungumzia suala la changamoto za maisha huku akidai kuwa suluhu ya masaibu ambayo mtu hupitia ni kifo tu.

image
na Radio Jambo

Habari13 October 2021 - 06:58

Muhtasari


•Baba huyo wa watoto wawili amezungumzia suala la changamoto za maisha huku akidai kuwa suluhu ya masaibu ambayo mtu hupitia ni kifo tu.

•Ujumbe wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 28 umeacha wengi na maswali chungu nzima haswa kuona kuwa hivi majuzi alizungumzia suala la kukosa kushikwa  mkono na wasanii wenzake katika mradi wa kuzindua albamu yake.

Zikiwa zimesalia siku chache tu albamu yake mpya izinduliwa, wasiwasi umeibuka kuhusu hali ya kisaikolojia ya mwanamuziki Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul.

Ujumbe wa hivi karibuni wa msanii huyo kwenye mtandao wa Instagram umeibua wasiwasi miongoni mwa mashabiki kwamba huenda amekabiliwa na msongo wa mawazo.

Kwenye ujumbe huo, baba huyo wa watoto wawili alizungumzia suala la changamoto za maisha huku akidai kuwa suluhu ya masaibu ambayo mtu hupitia ni kifo tu.

"Suluhu ya uchungu na shida ni kifo. Wakati mwingine huwa tunakabiliwa  na changamoto ambazo ni zaidi ya uwezo wetu". Sikuwahi elewa maana ya msongo wa mawazo lakini sasa najua" Willy Paul aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 28 umeacha wengi na maswali chungu nzima haswa kuona kuwa hivi majuzi alizungumzia suala la kukosa kushikwa  mkono na wasanii wenzake katika mradi wa kuzindua albamu yake.

"Kimbia mbio yako, siku 11 zimebaki kabla albamu kubwa zaidi itolewe, Halisi hutambua halisi.. kusema ukweli ihitaji usaidizi wa kinafiki kwa hii. Hapana!! nilizaliwa pekee yangi na nitazikwa pekee yangu. Kama uko na Mungu upande wako hauhitaji binadamu yeyote.. wale wanajikia kunisaidia karibuni.. wacha tutengeneze historua. Mwanaume mmoja dhidi yao wote" Willy Paula aliandika.

Hata hivyo hapo wasanii wengi nchini wanajulikana kutumia mbinu tofauti tofauti kutafuta kiki haswa wanapotazamia kutoa ngoma mpya na huenda ujumbe wa Paul ukawa moja ya mbinu zake anapopanga kuzindua albamu yake hivi karibuni.

Msanii huyo anayependa kujitambulisha kama 'Bwana Mkunaji' anatazamia kutoa albamu yake 'The African Experience' wiki ijayo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved