logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto wetu alikufa ndani ya tumbo kutokana na shinikizo la damu-DJ Mo

Huku akizungumzia jinsi wanaendelea na maisha baada ya kumpotea mtoto wao alisema;

image
na Radio Jambo

Burudani18 October 2021 - 13:13

Muhtasari


  • Mcheza santuri DJ Mo,amefichua mtoto wao alikufa kwenye tumbo, kwa hivyo ilibidi mkewe Size 8 afanyiwe upasuaji ili kuondoa mabaki

Mcheza santuri DJ Mo,amefichua mtoto wao alikufa kwenye tumbo, kwa hivyo ilibidi mkewe Size 8 afanyiwe upasuaji ili kuondoa mabaki.

Size 8 alipoteza ujauzito wake wiki chache zilizopita kwa sababu ya shinikizo kubwa sana la damu wakati wote wa ujauzito.

Akizungumza na Mpasho, Mo alishiriki;

"Alikuwa na ujauzito wa miezi mitano wakati tulitangaza habari. Wakati wowote anapopata ujauzito kawaida hupata shinikizo la damu kwa hivyo kwa miezi mitano, haikuwa rahisi.

Shinikizo likawa kubwa sana na mtoto akafariki na ikabidi afanyiwe upasuaji siku inayofuata vinginevyo tungeweza kuwapoteza wote wawili.

Watu walidhani tuliavya ujauzito lakini alikufa tumboni kwa sababu ya shinikizo la damu," Alisema Mo.

Huku akizungumzia jinsi wanaendelea na maisha baada ya kumpotea mtoto wao alisema;

"Unapoamini Mungu katika kila kitu inakuwa rahisi. Kikasha changu kimejaa hadithi za watu ambao wamepoteza hadi watoto 9, hivyo mambo haya ni ya kawaida. Kupata mimba na kujifungua  ni neema kutoka kwa Mungu. Huwezi kutabiri kile kinachoweza kutokea."

Kama wengi wanavyojua Mo aliacha kazi kwenye runinga ya NTV, Mo alidai kwamba ana kazi, na pesa aidi kuliko alivyokuwa kwenye runinga hiyo;

"Mimi nina kazi. Kwa kweli, nina pesa zaidi ya wakati nilipokuwa kwenye televisheni, ni kiasi gani unadhani NTV ilikuwa inanilipa mimi? "" Nimebadilisha brand yangu kidogo na sasa ninafanya ujasiriamali na pia ninafanya zabuni na mikakati ya masoko

Ikiwa unafikiri mimi sina kazi. Kweli, nilipata pesa kidogo NTVKuwa kwenye TV haimaanishi una pesa. Ni jukwaa tu kama nyingine yoyote. "


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved