Mbinu maarufu ambazo wasanii wa Kenya hutumia kutafuta kiki

Muhtasari

•Kunao baadhi ya wasanii wa hapa nchini wanaojulikana kupenda kiki sana ikiwemo Eric Omondi, Willy Paul, Bahati na wengineo.

Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Je wafahamu kiki ni nini?

Kulingana na Kamusi ya Kiswahili, neno kiki linamaanisha kupiga mpira kwa kutumia mguu.

Kwa lugha ya mtaani, kiki (clout) ni kitendo cha mtu haswa msanii kuanzisha drama ili kuibua gumzo ama kutaka kuangaziwa zaidi na watu.

Wasanii wengi, sio tu nchini Kenya bali kote dunia wanajulikana kutafuta kiki sana haswa wanapotazamia kutoa wimbo mpya ama kufanya tamasha.fulani.

Kunao baadhi ya wasanii wa hapa nchini wanaojulikana kupenda kiki sana ikiwemo Eric Omondi, Willy Paul, Bahati na wengineo.

Wasanii hutumia mbinu tofauti kutafuta kiki na zote hutegemea ubunifu wa anayetafuta kiki.

Hizi hapa baadhi ya mbinu za kawaida ambazo wasanii nchini Kenya wanapendelea kutumia sana:-

1. Mahusiano

Kwa kawaida ndoa ama mahusiano hufanyika kati ya wawili ambao wanapendana na wanatazamia kuanzisha familia pamoja.

Aghalabu watu wanapoamuua kujitosa kwenye mahusiano huwa wanaangaziwa sana na jamii wengi wakitaka kufuatilia mwelekeo wa mahusiano yale.

Hata hivo hapo awali mahusiano yametumika vibaya na baadhi ya wasanii ambao hujifanya kama kwamba wako kwenye mahusiano mradi tu waangaziwe na watu.

Mbinu hii imetumika sana nchini haswa wakati msanii wa kiume anatazamia kushirikiana na msanii wa kike kwenye wimbo.

Nadia Mukami aliwahi kudanganya kwamba ako kwenye mahusiano na jamaa mwenye asili ya Kihindi kisha ikafahamika baadae kuwa alitaka tu kumshirikisha kwa wimbo.

2. Utengano

Wakati kunao wasanii  ambao hujitosa kwenye mahusiano ili kuibua gumzo miongoni mwa watu, kunao wanandoa au wapenzi ambao haumua kujifanya kama kwamba wametengana almradi tu waangaziwe zaidi na watu.

Hii ni jambo la kawaida haswa miongoni mwa wapenzi mashuhuri ambao wanatazamia kufanya mradi pamoja kama vile wimbo ama video.

Mfano mzuri ni wakati mwanamuziki Bahati na mpenzi wake Diana Marua walikuwa wanapanga kutoa wimbo 'mtaachana tu' pamoja walifanya wanamitandao waamini kwamba wametengana.

EMB ENTERTAINMENT PRESENTS BAHATI FEATURING DIANA MARUA (@BAHATIKENYA & @DIANA_MARUA) #BahatiKenya #MTAACHANATUU Available on all digital platforms: http://smartklix.com/smartlink/?id=5bd62793&c=y WRITTEN BY KEVIN BAHATI AUDIO: EMB/ MESESI/ TEDDY B VIDEO: YOUNG WALLACE #BahatiReality #BahatiKenya #BeingBahati #BahatiMusic Subscribe to the channel for latest updates: http://bit.ly/BAHATIKENYA Watch more: BEING BAHATI- http://bit.ly/BeingBahati Best Of Bahati Music- http://bit.ly/BestOfBahatiMusic Best Kenyan Music- http://bit.ly/BestKenyanMusic Best Gospel Music- http://bit.ly/BestGospelMusic Follow me on: Facebook: https://www.facebook.com/Bahati-1410030652584881 Instagram:https://www.instagram.com/bahatikenya/ Twitter: https://twitter.com/BahatiKenya Digital distribution and Promotion by Ziiki Media

3. Ugonjwa/Ajali

Kunao wasanii ambao hupita mipaka na kujifanya kama kwamba ni wagonjwa ama wamehusika kwenye ajali ili tu waangaziwe na watu.

Ijapokuwa jambo hili ni la kusikitisha, kunao wasanii ambao kwa kawaida  hawajalishwi na matokeo ya matendo yao bora tu wanase umakini wa watu.

Mbinu hii ya kughadhabisha imetumika na wasanii wengi duniani.

Mapema mwaka huu Willy Paul alichapisha ujumbe mitandaoni kwamba amekabiliwa na msongo wa mawazo, hatua ambayo ilionekana kuwa kiki kwani alikuwa anapanga kuzindua albamu mpya 'The Black Experience'

4. Ugomvi

Kunao wasanii ambao hujifanya kama kwamba wanazozana ili tu kuibua gumzo na kuangaziwa na mashabiki wao.

Wasanii hawa hukorofishana hadharani ama mitandaoni  ili kunasa watu kisha baada ya kufanikiwa wanafanya mradi wa sanaa pamoja.

Mfano mzuri wa hivi karibuni ni wakati Willy Paul na Size 8 walijifanya kama kwamba wanazozana kisha wakashirikiana kutoa wimbo 'Lenga' pamoja mnamo mwezi Julai.

5. Kashfa (Scandal)

Kashfa ni jambo la aibu lililofanyika kwa siri ambalo limefichuka.

Kashfa huenda ikawa ya kimapenzi, kingono au ikahusiana na masuala mengine ya maisha.

Kunao wasanii ambao hujifanya kama kwamba wamehusika kwenye kashfa mradi tu wapate kufahamika zaidi ama kuangaziwa na watu.

Kashfa za kawaida miongoni mwa wasanii ni zile ambazo zinahusisha mapenzi, ngono au mitindo ya maisha.

Mfano mzuri ni tukio la miezi michache iliyopita wakati Eric Omondi alidai kampachika Miss P ujauzito kisha baadae wakatoa wimbo 'Baby Shower'

6. Uchokozi

Baadhi ya wasanii huchokoza wenzao  ili kuibua  gumzo na kuangaziwa zaidi na mashabiki kabla ya kutoa kitu kipya.

Willy Paul na Eric Omondi wanajulikana sana kutumia mbinu hii. Mara nyingi Eric Omondi ameonekana kuchokoza wasanii wenzake akikusudia tu kutafuta kiki. 

Wiki chache zilizopita Willy Paul alimchokoza mke wa Bahati, Diana ili kuuza albamu yake 'The Black Experience' zaidi.