(Video) Kiki tu!Miss P ashirikisha Eric Omondi kwa wimbo 'Baby Shower' siku chache baada ya madai ya ujauzito

Muhtasari

•Kwenye wimbo ambao unazungumzia sherehe ambayo hufanywa kama matayarisho ya kuzaliwa kwa mtoto, Miss P amemshirikisha Eric Omondi kama 'vixen'.

•Wimbo huu unajiri wakati mchekeshaji huyo anazungumzia sana mitandaoni kufuatia madai yake kwamba anashuku kuwa sio yeye baba mzazi wa mtoto wa Jackie Maribe kama inavyojulikana na wengi.

Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Ni wazi kwamba madai ya mchekeshaji Eric Omondi ya hivi majuzi kwamba alimpachika mwanamuziki Miss P ujauzito miezi mitano iliyopita yalikuwa ya uongo na walikuwa wanatafuta kiki tu. 

Siku chache tu baada ya mchekeshaji huyo ambaye amekuwa gumzo mitandaoni siku za hivi karibuni kudai kwamba alikuwa anatarajia mtoto pamoja na Miss P, mwanamuziki huyo ametoa wimbo  ambao unaoitwa 'Baby Shower'

Kwenye wimbo ambao unazungumzia sherehe ambayo hufanywa kama matayarisho ya kuzaliwa kwa mtoto, Miss P amemshirikisha Eric Omondi kama 'vixen'.

Miss P amewashukuru wote ambao walifanikisha kutengenezwa kwa wimbo huo ikiwemo Eric Omondi.

#MissP #Babyshower #Baby-daddy Miss P presents Her first single BABY SHOWER. BIG Thanks to everyone who made this possible. CREW AUDIO - JEGEDE ON THE BEAT VIDEO PRODUCER - ERIC OMONDI DIRECTOR - JIMMY KIMAITA DIRECTOR OF PHOTOGRAPHY - SAMMY EM. DECOR BY JOSEPHINE PRODUCTION ASSISTANT - CALVIN KLAKS SHOT ON LOCATION AT MALIA BAROQUE STYLIST - DIANA CHANZU DESIGNER - MELINA GOLD PHOTOGRAPHER -STORY ZA KAPEDO.

Wimbo huu unajiri wakati mchekeshaji huyo anazungumzia sana mitandaoni kufuatia madai yake kwamba anashuku kuwa sio yeye baba mzazi wa mtoto wa Jackie Maribe kama inavyojulikana na wengi.

Usiku wa Jumanne Omondi alidai kwamba alihakikisha kwamba ametumia kinga wakati aliposhiriki mapenzi na Maribe.

Alisema kwamba alishtuka sana wakati Bi. Maribe alimpigia simu miezi miwili baadae akimweleza kuwa alikuwa amebeba ujauzito wake ilhali kinga ilitumika wakati walipokuwa wanashiriki mchezo wa kitandani.

"Tulitumia kinga!!  Baada ya miezi miwili Jacque aliniambia kuwa ni mjamzito!! Mara moja nilimuuliza ikawaje ilhali tulitumia kinga?? Aliniambia kuwa hiyo haijalishi kwani mama ndiye hujua baba mzazi wa mtoto wake" Alidai Omondi.

Mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama alidai kuwa baada ya mtoto kuzaliwa aliagiza Maribe wafanye vipimo vya uzazi (DNA) ili athibitishe kuwa ndiye baba ya mtoto yule ila mtangazaji yule hakukubaliana na agizo lake.

"Takriban miezi minne baada ya mtoto kuzaliwa Jacque alinipigia simu akaniulia kama nitamsaidia kulea  ama nitakuwa maishani ya mtoto yule. Niliomba tufanye DNA ili nikubali kuwa maishani ya mtoto na nimsaidie kulea.  Alikasirika na akakataa ombi langu. Kwa miaka saba nimebembeleza Jacque akubali tufanye vipimo vya DNA lakini ameendelea kukataa!!" Alisema Omondi.

Omondi alisema atakubali kusaidia katika malezi ya mvulana huyo wa miaka saba iwapo tu Maribe atakubali wafanye vipimo vya DNA.