Msanii wa lebo ya muziki ya Legacy Records Entertainment na msanii chipukizi wa Afro Pop kutoka Tanzania Loui ametoa video ya kibao kipya ambacho kilikuwa kimesubiriwa sana na mashabiki mwishoni mwa mwaka.
Kibao hicho kinafahamika kama 'My Queen'.
Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya kuachia wimbo wake "Hennessy" ambao ulifanya vyema sana kwa kutazamwa zaidi ya milioni 4 kwenye mitandao ya YouTube na Kwenye mitandao mbalimbali na pia baada ya kuangusha ‘Selema Popo’ na mshindi wa tuzo ya DJ wa Afrika Kusini na mtayarishaji, Musa Keys.
"Video hii itapeleka kazi yangu kwenye video inayofuata. Tunaanza Mwaka kwa kiwango cha juu zaidi
Moja ya video bora zaidi kuwahi kupigwa na mkurugenzi mchanga na mahiri ambaye tunashiriki maono sawa
Video ni tofauti kidogo iliyojaa nyakati tofauti za furaha ambazo huambatana na wimbo na sauti yangu
Mbali na kuonyesha kipaji changu na uwezo nilionao wa kuleta mabadiliko katika Tasnia hii, mimi tu nilitaka kuonyesha ulimwengu jinsi nchi yangu ilivyo nzuri
Huu ni Wimbo mzuri na ninaomba kila mtu atazame, afurahie na ashiriki wimbo huu bora wa Afro Bongo” Alisema Loui.