Mwanablogu na mfanyibiashara, Thee Pluto amesema kwamba bado penzi lake na Felicity Shiru lipo imara licha ya utofauti wa dini kati yao.
Akizungumza katika mahojiano na wanablogu huko Mombasa, Pluto alisema kwamba watu hawaingii katika mapenzi kwa sababu ya dini na hiyo haipaswi kuwa sababu ya watu kutooana.
"Ndugu yangu, kwani watu wanaoa kwa sababu ya dini? Watu wakipendana wanaona tu," Pluto alisema.
Pluto alisema kwamba mapenzi yanatoka rohoni na kuwa kuna misingi mingine mingi ambayo kwayo mtu anapaswa kumpenda mtu.
Kauli hii inajiri siku chache baada ya madai kwamba wawili hao walikuwa hawapo pamoja tena, huku Pluto akisema kwamba hizo ni propaganda za mashabiki katika mitandao.
Ifahamike kwamba wawili hawa walikuwa wametengana kipindi cha nyuma ila wakafanikiwa kusuluhishwa mambo yao na kurejea pamoja.
Katika siku za hivi karibuni, Thee Pluto ameonekana kuweka siri sana mambo mengi kuhusu mahusiano yake, kwa kile kinachotajwa kama kulinda penzi lao kutoka kwa watu wanafiki.