logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwijaku asema yeye ndiye mshauri wa Diamond Platnumz

Mwijaku amesema kwamba yeye ndiye mshauri mkubwa wa Diamond Platnumz.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 March 2022 - 08:25

Muhtasari


  • • Mwanahabari Mwijaku amesema kwamba yeye ndiye mshauri mkuu wa Diamond Platnumz.
  • • Amesema kwamba anachukia sana Simba anapokosa kufuata ushauri wake.
Instagram, KWA HISANI

Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Mwijaku sasa anasema kwamba yeye ndiye mshauri mkubwa wa Diamond Platnumz.

Mwijaku amesema kwamba baadhi ya maamuzi makubwa na ya maana anayoyafanya Simba, anapata ushauri kutoka kwake.

Aliongezea kwamba kuna mambo mengi wamezungumza ila Diamond hawezi kuyaweka hadharani.

"...Hawezi kuonyesha mawasiliano yangu mimi na yeye kwa mtu yeyote,mshauri wake mkubwa ni mimi. Si mmemsikia kwenye chombo chake cha habari kaongea," alisema Mwijaku.

Alikiri kwamba ameonekana kuwa mkali na kumsuta Simba kwa sababu anafanya maamuzi ndivyo sivyo.

Mtangazaji huyo alisema kwamba yeye ni miongoni mwa Watanzania wachache ambao wana kisomo kikubwa na hivyo hafai kuchukuliwa poa tu.

Aidha alisema kwamba Diamond Platnumz hayupo kwenye orodha ya wanamuziki kumi  bora Afrika.

Ifahamike kwamba kwa kipindi kirefu sasa, Mwijaku ameonekana kuegemea upande wa Alikiba na Harmonize akisema kwamba ndo wanaoelewa muziki na gemu la burudani kwa ujumla.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved