logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sifanyi show, hawawezi kunilipa - Hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto amesema kwamba mapromota wengi wanawachukulia poa wasanii.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 April 2022 - 08:07

Muhtasari


  • • Hamisa Mobetto amesema kitendo cha mapromota kumchukulia poa kimemsabbabishia yeye kukosa kufanya show.
  • • Amesema kwamba maamuzi hayo yanalenga kuepusha mvutano kati yake na washikadau wa burudani.
Instagram, KWA HISANI

Msanii na mfanyibiashara kutoka Tanzania Hamisa Mobetto ameweka wazi sababu zake za kutofanya shows.

Mobetto amesema kwamba mapromota wengi wanawachukulia poa wasanii na kuwalipa kiasi kidogo cha hela.

Kulingana naye, mapromota wengi wanawadhulumu wasanii baada ya kufanya show wakidai kwamba wanaitisha kiasi kikubwa cha pesa ambacho

"Kwahiyo unaombaje msanii aje kufanya shoo, halafu baada ya kazi unadai ni ghali sana na kumfukuza eti unaweza kupata msanii mwengine," Mobetto aliandika.

Msanii huyo amekashifu washikadau wanaowakosea heshima wanamuziki akisema kwamba hiyo ni ajira kama nyingine.

Hamisa alikiri kwamba anafanya muziki kujifurahisha tu kwa sababu hataki kugombana na mapromota wa nchini humo ambao pia hawawezi kumudu bei yake ya kupanda jukwaani.

Ifahamike kwamba Hamisa Mobetto ni moja kati ya wasanii wa kike ambao wanazidi kufanya vizuri ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved