logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Willy Paul afichua sababu ya kuwa na CCTV nyumbani mwake huku akiiomba Safaricom iongeze mapato yake

Kulingana na willy Paul, kuna baadhi ya marafiki wana tabia ya kusema uongo

image
na Radio Jambo

Habari22 April 2022 - 13:55

Muhtasari


  • Kulingana na msanii huyo mwenye utata, Rais Uhuru aliagiza kuongezwa mara moja kwa asilimia ya mapato ya skiza
Willy paul

Msanii Willy Paul amefichua ni kwa nini ana CCTV kwenye nyumba yake yote.

Mwanamuziki huyo alifichua haya alipokuwa akiendelea na kuomba kampuni ya safaricom kuongeza mapato yake ya skiza.

Kulingana na msanii huyo mwenye utata, Rais Uhuru aliagiza kuongezwa mara moja kwa asilimia ya mapato ya skiza.

Hata hivyo, hajawahi kuona mabadiliko yoyote kwenye mapato yake. Willy Paul alishiriki machapisho marefu kwenye hadithi zake za Instagram akihutubia kwa nini ana CCTV.

Kama inavyoonekana kwenye machapisho, Willy Paul aliamua kusakinisha cctv katika nyumba yake yote kwa sababu ya marafiki zake na aina ya wageni ambao yeye huwakaribisha kila mara.

Kulingana na willy Paul, kuna baadhi ya marafiki wana tabia ya kusema uongo hivyo basi kulazimisha kujithibitisha kwa usaidizi wa kanda za cctv.

Katika chapisho lililofuata, Willy Paul aliomba Safaricom Kuongeza mapato yake ya skiza. Alidai kuwa Rais aliongeza asilimia hiyo hivyo alitarajia ongezeko la mapato.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved