Mfanyibiashara Nicola Tradi amefikishwa mahakamani ili kijubu mashtaka ya dhuluma dhidi mpenzi wake Chantal Grazioli.
Kulingana na karatasi ya mashtaka, kisa hicho kilitokea katika mtaa wa Kilimani, kaunti ya Kiambu.
Traldi alikanusha mashtaka ya kumshambulia mpenzi huyo wake na kumvunja mguu wa kushoto.
Wakili wa mlalamishi alitaka mahakama imzuie mshtakiwa kufikia mlalamishi kwa njia yoyote ile akidai kwamba walikuwa wameanza kumtafuta hadi kwake, kitu ambacho kilimuogopesha na akahamia pahali pa usalama.
Haya yalijiri baada ya Wakili wa Chantal kufahamisha mahakama kuwa , mamake Traldi alikuwa anatafuta mteja wake hadi usiku.
Hata hivyo wakili wa upande wa utetezi alisema hatua ya familia ya mshtakiwa huenda ni kwa sababu walijaribu kutafuta suluhu nje ya mahakama..
Hakimu aliamuru kwamba mshtakiwa anapaswa kuacha stakabadhi zake za usafiri na mahakama. Pia haruhusiwi kuwasiliana na mlalamishi au familia yake.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe Septemba 13 mwaka huu.
Eric Omondi ambaye alikuwa mpenzi wa Chantal wa zamani katika taarifa yake, alimkashifu Traldi kwa kitendo hicho ambacho kilishangaza watu wengi .
“Mwanaume yeyote anayempiga mwanamke ni MUOGA!!! Nicola Traldi ni Mwoga. Ni Mdhaifu na Hajiamini. Nguvu za mwanamume hujidhihirisha pale ANAPOMLINDA mwanamke na si anapomwekea mikono,” sehemu ya chapisho la Eric Omondi.
Siku ya Ijumaa, Omondi alipakia video ya dakika moja akimshutumu Traldi kwa kumshambulia Chantal - akisema kwamba hakuna sababu ya mwanamume kumpiga mwanamke.
Mnamo Mei, 2019 Eric Omondi na Chantal walikatiza uhusiano wao wa miaka minne kupitia machapisho marefu kwenye Instagram. Wakati huo, Omondi alisema kuwa alimfahamu Chantal kwa muda mrefu na kukuwa na yeye pamoja ilibadilisha kabisa maisha yake, kwani alimtakia kila la kheri maishani.
"Nataka kukujulisha kuwa nitakuwa hapa kwa ajili yako wakati wowote, kila wakati.Uweze kung'aa, Ung'ae kama Malaika ulivyo. Nitakukumbuka kila dakika...Kila wakati. Wewe ndiye jambo bora zaidi lililonipata !!! Na kwa wale wadau wadaku, Chantal and I are okay. Tulikuwa marafiki kwa muda mrefu kabla ya kukuwa wapenzi na Urafiki wetu unabaki maishani,”Alisema Omondi katika chapisho wake wa kutengana mnamo Mei 2019.