Msanii wa Injili Daddy Owen ajenga makao ya watoto walemavu huko Eldoret

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo amekuwa akifanya kazi ya kuwasaidia watoto walemavu wanaohitaji upasuaji.

•Baada ya kurejea Nairobi, alitembelea Baraza la Kitaifa la Watu Wenye Ulemavu.

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen amefichua mipango ya kuzindua makao ya watoto walemavu mjini Eldoret.

Aliwatangazia mashabiki wake kuhusu jengo hilo kwenye Instagram yake,alisema kuwa mradi huo utazinduliwa Agosti mwaka huu.

"Badala ya kuwa binadamu tu, kuwa na Utu pia...... Ukaguzi wa mchakato unaoendelea wa mradi wa makazi ya watoto utazinduliwa mwezi wa Agosti mjini Eldoret. Taarifa rasmi zitafuata hivi karibuni na tarehe za uzinduzi." Owen alisema.

"Kusudi langu maishani ni kusaidia watu wenye ulemavu, zaidi, watoto wenye ulemavu." aliongeza.

Mwanamuziki huyo amekuwa akifanya kazi ya kuwasaidia watoto walemavu wanaohitaji upasuaji.

Kila mwaka, mwimbaji Owen huwa na tuzo za Malaika Tributes kusherehekea mashujaa ambao hawajatungiwa nyimbo.

Wakati wa tuzo za miaka zilizopita, Owen alidokeza jinsi wazo la kuanzisha sherehe hilo lilivyotokea.

Mwaka 2012, nilifanya wimbo wangu wa ‘Mbona’ nikishirikisha Denno, na tukiwa kwenye ziara nchini Kenya, tulikutana na watu kadhaa nchini,” alisema.

"Nilikutana na kijana ambaye alikuwa mhandisi lakini alikuwa kwenye kiti cha magurudumu. Jamaa huyo alinipa changamoto."

Baada ya kurejea Nairobi, alitembelea Baraza la Kitaifa la Watu Wenye Ulemavu.

Ilikuwa ni jambo la kushangaza kuona watu wanafanya mambo mengi licha ya ulemavu wao, kila mwaka tunapata washindi 10 kila mmoja akienda na hundi ya Ksh.100,000” alisema.

"Wanatumia pesa  hizo  kwa kujijenga. Tumekuwa na hadithi nzuri, tumetunuku watu tofauti nchini."aliongeza.

Owen alisimulia jinsi tukio hilo linamkumbusha kuhusu unyanyapaa aliopitia baada ya kupoteza jicho lake moja mwaka wa 2002.

Mmoja wa walionufaika na tuzo za Malaika Tribute ni Ignatius Ogeto, almaarufu DJ Euphorique, ambaye ni mmoja wa waimbaji bora zaidi nchini licha ya kuwa  mlemavu.

"Wakati mmoja, nilikutana na DJ Euphorique na akaonyesha nia ya kuwa DJ. Alisema alihitaji mashine. Niliwaambia marafiki kuwa anahitaji 500k, walichangisha pesa. Euphoric ni zao la Malaika." Owen alisema.

 

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN