Rais Museveni amwandikia mkewe ujumbe wa kipekee anapoadhimiasha miaka 74

Muhtasari
  • Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameandika ujumbe mtamu kwa mkewe anapofikisha umri wa miaka 74 leo
  • Museveni pia alifichua kuwa Mama Janet amejitolea kwa Mungu, familia ya Museveni na watu wote wa Uganda
Rais wa Uganda Museveni na mkewe Mama Janet
Image: YOWERI MUSEVENI/TWITTER

Ni nadra sana kwa wakati huu wa sasa wanandoa kudumu kwenye ndoa zao hadi,wazeeke au kifo kitakapowatenganisha.

Swali kuu ambalo linasalia akilini mwa watu wengi, sababu kuu ya ndoa za karne hii ya sasa kuvunjika kila kuchao ni ipi?

Kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kila mwaka ukiwa na afya njema, na uko mzima ni moja wapo ya zawadi kuu ambayo kila mmoja anapaswa kumshukuru Mungu Kwalo.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameandika ujumbe mtamu kwa mkewe anapofikisha umri wa miaka 74 leo.

Kupitia akaunti yake rasmi ya twitter, Museveni alimpongeza Mama Janet huku akimtakia miaka mingi zaidi ya afya njema, mafanikio na furaha.

Museveni pia alifichua kuwa Mama Janet amejitolea kwa Mungu, familia ya Museveni na watu wote wa Uganda.

"Nampongeza sana Maama Janet kwa kufikisha umri wa miaka 74, namshukuru Mungu kwa uhai wake, asante Janet kwa upendo na kujitolea kwako kwa Mungu, familia yetu na wananchi wa Uganda, akupe miaka mingi zaidi ya afya njem,"Museveni aliandika.