logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Juliani asema alipoteza dili 2 wakati wa sakata la kumchukua Ng'ang'a kutoka kwa Mutua

Mwanzoni mwaka jana Sakata hilo lilisababisha kupoteza dili mbili ambazo nilikuwa nimepanga kufanya - Juliani.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 September 2022 - 08:59

Muhtasari


  • • Juliani alisema sakata la kuachana kwa Ng'ang'a na gavana Mutua na yeye kuwa mziba pengo hilo lilimletea njaa katika maisha yake ya usanii.
  • • Alisema alipoteza dili mbili ila akasisitiza kwamba kwa sasa maisha yake yako sawa na kila kitu kiko vizuri.
Juliani na mke wake Lilian Nganga

Msanii Jukiani amefunguka jinsi Sakata la mkewe Lilian Ng’ang’a na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua lilihitilafiana na riziki yake katika tasnia ya usanii mwishoni mwa mwaka jana.

Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa mwaka jana ndio Sakata hilo lilizaliwa pale amabpo Ng’ang’a na Mutua waliweka wazi kuvunja mahusiano yao ambayo mpaka hapo walikuwa wametembea umbali wa miaka 10 kama wapenzi pamoja pia na kuanzisha miradi kadhaa.

Miezi michache tu baada ya Mutua na Ng’ang’a kuachana, Juliani alijipata kwenye picha ambapo alihusika kama mtu wa kuziba nafasi Mutua aliacha kwenye maisha ya kimapenzi ya Ng’ang’a.

Kuingia katika mahusiano na Lilian kulimsababishia figisu vikali kutoka kwa watu mitandaoni ambao waligawanyika katika makundi baadhi wakimpongeza kwa kufanikiwa kumng’atua Ng’ang’a kutoka kwa Mutua huku wengine wakimkashfu kwa kuchukua uamuzi huo.

Msanii huyo sasa kwa mara ya kwanza amefunguka jinsi gumzo hilo lilimletea njaa katika maisha yake kama msanii.

Juliani akizungumza na Mpasho alisema kuwa ilimsababishia kupoteza madili mawili ya shoo ambazo alikuwa anatarajia kufanya na kujizolea riziki.

“Mwanzoni mwaka jana Sakata hilo lilisababisha kupoteza dili mbili ambazo nilikuwa nimepanga kufanya. Kwa sababu watu walidhani kama nilikuwa nafanay mzaha au nini na ndio nilipoteza dili mbili. Mwaka jana mambo hayo yalipozuka nilipoteza dili hizo lakini iko tu sawa, maisha lazima yaendelee” Juliani alisema.

Msanii huyo alizidi kusisitiza kwamba maneno yake mitandaoni kuwa amekuwa maskini ni mchezo tu alikuwa anafanya ili kukabiliana na wale waliokuwa wanamfanyia mchezo pia mitandaoni.

Alisema yeye amekejeliwa kwa miaka mingi na hata sasa hivi watu wakijaribu kumkejeli haoni kama ni ishu kubwa kwani aliyapitia mengi miaka ya awali akiwa katika mtaa wa mabanda wa Dandora na ameshazoea sasa hivi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved