logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Bila wewe moyo wangu ungevuja damu!" Mauzo amsherehekea mkewe Vera Sidika

Mwanasoshalaiti Vera Sidika anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

image
na Samuel Maina

Burudani30 September 2022 - 08:10

Muhtasari


  • •Brown Mauzo ni miongoni mwa waliojiunga na Vera kusherehekea siku hii maalum katika maisha yake.
  • •Mauzo alimtakia mpenziwe kheri ya siku ya kuzaliwa na na kumweleza jinsi anavyotazamia kuwa naye siku zote za maisha yake.

Leo hii, Septemba 30, mwanasoshalaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Vera ambaye alijizolea umaarufu mwongo mmoja uliopita baada ya kushirikishwa kwenye video ya wimbo 'You Guy' wa P-Unit anaadhimisha kutimiza miaka 33. Wanamitandao na watu wa karibu wameendelea kumsherehekea mwanasoshalaiti huyo na kumwandikia jumbe za kheri ya siku ya kuzaliwa.

Mume wake Brown Mauzo ni miongoni mwa waliojiunga naye kusherehekea siku hii maalum katika maisha yake. Ametumia fursa hiyo kumsherehekea kama mke bora.

"Unapopuliza mishumaa kwenye keki ya siku yako ya kuzaliwa, nataka kukuambia jinsi gani wewe ni mke mzuri," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mauzo alimtakia mpenziwe kheri ya siku ya kuzaliwa na na kumweleza jinsi anavyotazamia kuwa naye siku zote za maisha yake.

"Bila wewe katika maisha yangu, moyo wangu ungekuwa umevuja damu. Pamoja na wewe, ninatazamia maisha mazuri mbeleni. Heri ya kuzaliwa Mke wangu @queenveebosset," alisema.

Vera  alijibu kwa kumshukuru mzazi huyo mwenzake na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Aww, shukran mpenzi. Nakupenda sana mpenzi wangu," alijibu.

Wanandoa hao wawili wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takriban miaka miwili sasa. Walikutana Agosti 2020 na kuanza kuchumbiana kabla ya kubarikiwa na mtoto wao wa kwanza mnamo Oktoba 2021.

Kabla ya kuchumbiana na Mauzo, Vera aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Otile Brown, Dkt Jimmy Chansa kutoka Tanzania, Yommy Johnson kutoka Nigeria miongoni mwa wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved