Hatua ya mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna kumsherehekea mama ya Diamond Platnumz kwa njia ya kipekee imewasha moto mkubwa usiozimika bongo.
Jumatano jioni, Bi Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote alifichua zawadi za bei ghali ambazo mama huyo wa mjukuu wake alimpa hivi majuzi kwa siku yake ya kuzaliwa ambayo ilipita miezi miwili iliyopita. Kifurushi cha zawadi kilijumuisha pesa za Dola ya Marekani na Shilingi ya Tanzania, maua na bidhaa ghali ya urembo.
Kifurushi hicho pia kiliambatanishwa na barua ambapo Tanasha alionekana kumuomba radhi mama mkwe huyo wake wa zamani kwa kuchelewa kwake kumsherehekea.
“Mama, kitu kidogo kwa kutotimiza ahadi yangu. Natumai unaipenda. Heri ya siku ya kuzaliwa mama!! Mwenyezi Mungu akubariki daima. Upendo, T,” ujumbe kutoka kwa Tanasha ulisomeka.
Katika majibu yake, Mama Dangote alionekana kuishiwa kabisa na maneno kutokana na upendo mkubwa alioonyeshwa na mama huyo wa mjukuu wake na kumshukuru tu sana kwa hilo.
“Duuuh natoka zangu site nakutana na Surprise ya zawadi yangu ya birthday kutoka kwa Mama Tom kaka @tanashadonna yani sina cha kusema ila nasema Alhamdullillah,” Mama Dangote aliandika chini ya video ya zawadi za Tanasha ambazo aliziweka kwenye Instagram.
Punde baada ya mamake Diamond kufichua alichomfanyia Tanasha Donna, sehemu ya maoni ya chapisho lake iligeuka kuwa jukwaa la mjadala huku wanamitandao wakijumuika kutoa hisia kemkem kuhusu hatua ya mwimbaji huyo wa Kenya.
Kundi la wanamitandao walionekana kuhusisha kitendo cha Tanasha Donna na kufufuka kwa mahusiano yake na bosi wa WCB ambayo yaligonga mwamba takriban miaka mitatu iliyopita huku baadhi hata wakiwataka warudiane tayari.
“@mama_dangote @diamondplatnumz @_esmaplatnumz Mke Ni @tanashadonna Na Ndo Anaendana Na Nyie Binti Mzuri Anaonekna Mpole Japokuwa Sijakaa Nae Ila Msichana Mwenye Hadhi Ya @diamondplatnumz Ni Huyo Ana Kila Sifa Ya Kuwa Na Star Wetu Wa Duniani Ukiwa Star Lazma Na Umiliki Anayemiliki. Wako Bwana Binti Mzuri Anakila Sifa Yani Ya Kuwa Na BIG πππ,” de_souza_10 alitoa maoni yake chini ya post ya Mama Dangote.
@marynfatma alisema, “Huyu ndio mkwe wetu tu siku haijafika.
Baadhi ya wanamitandao wengine waliotoa maoni yao chini ya chapisho hilo pia walionekana kupendekeza kuwa wakati wa Zuchu umekwisha na ni wakati wa yeye kuondoka. Malkia huyo mzaliwa wa Zanzibar amedaiwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond kwa takribani miaka miwili iliyopita.
Madai ya Zuchu kutakiwa kwenda yalizidi pale Mama Dangote alipo-pin maoni ya mwanamtandao aliyependekeza Tanasha arudi ili malkia huyo wa bongo achekwe.
"Tanasha diamond amuone tuβ€οΈβ€οΈβ€οΈ mzanzibar achwe tucheke," @rash.eed2714 aliandika, maomni ambayo mamake Diamond alionekana kukubaliana nayo kwa kupin kwenye post yake.
Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao wengine;-
@nami_g10: Zuchu kaanza kufanyiwa vituko akufukuzae hakwambii toka. Af hata hajatuma tanasha hyo zawad imetoka kwa mondi mwnyw ππππππππ
mugambigeorgina: Wacheni ushamba ,that's her Child Grandmother's .She is an independent woman with her own path .Bibi will always be Bibi pthoo..
latifahbrown8: Pls zuchu move on you are famous enough you donβt need diamond anymore this family will make your life so miserable you will not concentrate on your music this family donβt have any value the only think about moneyππ½π
leemaudaku: Wakubwa washaelewa ππππππ mchezo si mshaujua ?
its_shekinglee:Ndo huyu ndo wanamsifiaga kamove on au?π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£