logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwakani Hamisa Mobetto asipokuwa Best Female Tanzania naacha kuimba - Harmonize

“Yaani mwakani Hamisa asipokuwa Best Female hapa Tanzania, naacha kuimba,” Harmonize.

image
na Davis Ojiambo

Burudani16 October 2023 - 10:24

Muhtasari


  • • “BFF wangu hakuhudhuria shoo yangu lakini kila kitu kiko sawa, tulikuwa na muda mzuri ila najua washauri ni wengi mno, eti anakutumia ajaze shoo yake,” alisema.
Harmonize na Hmisa Mobetto.

Msanii Harmonize ameendelea kutuma pasi zake za kuvizia vizia kwenye lango la mwanasosholaiti  Hamisa Mobetto bila kufa moyo licha ya Mobetto kumkanya mara si moja.

Hata baada ya Mobetto kumtosa Harmonize kwa kudinda kuhudhuria kwenye shoo yake Dar es Salaam wikendi, Harmonize hajaonesha ubaya wowote na amezidi kusisitiza kwamba mrembo huyo mama wa watoto wawili bado atasalia kuwa rafiki wake wa karibu, BFF.

Harmonize amemsifia Mobetto pakubwa na hata kutoa ahadi kwamba ifikapo mwaka 2024 na Hamisa Mobetto bado hajatajwa kama mwanamke mrembo Zaidi nchini Tanzania, basi yeye yuko radhi kustaafu katika kuimba muziki.

“Yaani mwakani Hamisa asipokuwa Best Female hapa Tanzania, naacha kuimba,” Harmonize alimwambia Mwijaku kabla ya kufunga mlango wa gari lake la kifahari.

Akizungumzia Mobetto kutohudhuria shoo yake, Harmonize alisema bado mambo yao yako sawa wala hilo halitakuwa mzizi wa chuki, huku akiwalaumu watu kwa kumshauri Mobetto kutohudhuria kuwa angemfaidi bure msanii huyo.

“BFF wangu hakuhudhuria shoo yangu lakini kila kitu kiko sawa, tulikuwa na muda mzuri ila najua washauri ni wengi mno, eti anakutumia ajaze shoo yake,” alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo wa Konde Gang kuonesha mapenzi yake kwa Hamisa licha ya kufahamu fika kwamba mrembo huyo kwa sasa ni mtu na mpenzi wake na kutokea nchini Togo kwa jina Kevin – mjasiriamali wa migahawa nchini Uchina.

Hivi majuzi, Harmonize alisema kabla ya kuondoka zake kwenda ziara yake ya Marekani, atakuwa anapita kwenye mitaa na pindi atakapooona chombo chochote chenye picha yake na ile ya Hamisa Mobetto, atatoa shilingi laki 5 za kitanzania kwa kila picha.

Alisema kwamba hiyo itakuwa ishara moja ya kurudisha shukrani kwa mashabiki wake ambao wanazidi kumuonesha mapenzi yasiyo na shruti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved