Kwa muda mrefu mchekeshaji na mkuza maudhui Oga Obinna amekuwa akimfukuzia mwanasosholaiti Amber Ray kwa nia na lengo la kumchukua kama mpenzi wake.
Obinna amekuwa akionesha nia hii hata wakati mrembo huyo mama wa watoto wawili alikuwa katika penzi la hadharani na baba wa binti yake, Kennedy Rapudo.
Kumfuata kwake kulichochewa hata Zaidi baada ya Amber Ray na Rapudo kuweka wazi hivi majuzi kwamba wameachana.
Obinna alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kujitokeza bila woga na kusema kwamba alikuwa yayari kutumia fursa ya kuondoka kwa Rapudo ili kumchumbia Amber Ray.
Lakini Amber Ray kwa mara ya kwanza amemjibu na kumwambia kwamba hawezi hata sekunde moja kukubali penzi la mchekeshaji huyo, akitaja chanzo kuwa babymama wake ambaye ni kisirani.
“Obinna hata siwezi, haiwezi kabisa kwanza vile nasikia babymama wake ako stressfull, mimi sitaki drama za babymama, lakini namtakia kila la kheri, ni jamaa mzuri tumekutana mara nyingi tu na tumefanya kazi nyingi pamoja,” Amber Ray alisema.
Mrembo huyo alisema kuwa yeye katika maisha yake hajawahi tafuta mwanaume kwani mar azote amekuwa akifuatwa na wapenzi wake wote ambao amechumbiana na yeye.
Pia aliweza kuzungumzia video iliyomuonesha akiwa na mbunge wa Nyaribari Chache Zaheer Jhanda wakati wa ziara yake Kisii.
Ray alisema kwamba ni kweli Jhanda waliwahi kuwa wapenzi nyakati za nyuma lakini penzi lao lilikuja likaisha na kwa sasa ni marafiki tu, pia akafutilia mbali uwezekano wa kurudiana naye.