Jaribio la hivi majuzi la Grand P la kumbeba mpenzi wake Eudoxie Yao mgongoni lilimalizika vibaya kwani mwimbaji huyo tajiri wa Guinea alianguka vibaya mara baada ya mwanasholaiti huyo wa Ivory Coast kupiga hatua ya kupanda mgongoni mwake.
Katika video ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, Grand P ambaye jina lake halisi ni Moussa Sandiana Kaba alionekana akilalamika vikali baada ya kushindwa kumbeba mpenzi huyo wake ambaye bila shaka anaonekana kuwa mkubwa zaidi yake mara kadhaa.
"Ah mwanamke, mbinguni hatarini Azaya Yoo," mwimbaji huyo tajiri alisema kuhusu tukio hilo.
Katika video hiyo, wapenzi hao wawili walionekana wakibishana kuhusu mahali tatizo lilitokea na kujaribu kujadiliana kuhusu jinsi ya kufanikisha kabla Grand P hajafanya jaribio la pili la kumbeba mrembo huyo mwenye mwili mkubwa wa kuvutia.
Jaribio la pili hata hivyo lilishindwa pia.
Grand P ni mwimbaji maarufu kutoka Afrika Magharibi na anajulikana sana kwa mwili wake mdogo wa kipekee na sauti yake ya mtoto. Licha ya kuwa tayari ana umri wa miaka 30, mwimbaji huyo anasemekana kuwa na urefu wa sentimita 106 tu.
Mpenzi wake Eudoxie Yao hata hivyo ana mwili mkubwa uliopinda, jambo linalowafanya kuwa wanandoa wa kipekee sana.
Bi Eudoxie Yao, katika mahojiano ya hivi majuzi na kituo cha runinga cha Ghana alifunguka kuhusu sababu ya misukasuko mingi katika uhusiano wake na Grand P.
Mrembo huyo alifichua kuwa amewahi kuachana na Grand P na kurudiana naye mara kadhaa tangu waanze kuchumbiana takriban miaka minne iliyopita.
Alidai kuwa mwanamuziki huyo bwenyenye ana upendo mkubwa kwa wanawake, jambo ambalo limemfanya amuache mara kadhaa wakati wa uhusiano wao.
"Tumechumbiana tangu 2019. Tunaachana, Tunarudiana. Tunaachana tena na kurudiana.. Anapenda wanawake sana,” Grand P alisema katika mahojiano na Joy News.
Grand P ambaye alikuwa pamoja na mpenzi wake wakati wa mahojiano hayo hata hivyo alikuwa mwepesi sana kukanusha madai ya kuwapenda wanawake sana.
"Hapana! Hapana! Ni Mungu pekee ndiye anayejua,” Grand P alisema.
Huku akizungumzia uhusiano wao, Bi Yao aliweka wazi kuwa licha ya wao kutofunga ndoa rasmi, upendo ni wa kweli kabisa.
Wakati wa mahojiano, Grand P ambaye ni Muislamu hata hivyo alifichua kuwa nia yake ni kuoa takriban wanawake wanne.
“Nataka kuoa wanawake wanne. Si mimi niliyesema hivyo, ni baba yangu (Mungu) anayesema hivyo,” alisema.
Eudoxie Yao hata hivyo alikuwa mwepesi wa kutokubaliana na wazo hilo akisema, "Ikiwa atathubutu, tunaachana."
Grand P hata hivyo alidokeza kuwa hataogopa sana kumpoteza mwanamke huyo mwenye u