logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Esther Musila na Guardian Angel waadhimisha miaka 2 katika ndoa

"Hii imekuwa safari nzuri, na mimi bado ni bibi arusi wako" Musila alimwambia Angel.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 January 2024 - 12:45

Muhtasari


  • • “Tukitafakari juu ya safari yetu, kuna mambo 3 ambayo yatadumu daima; IMANI, UPENDO, na TUMAINI. Kubwa kwetu ni UPENDO." Musila alisema,
  • • Wawili hao wamekuwa wakionesha mapenzi yao hadharani licha ya kukashifiwa kutokana na utofauti mkubwa wa umri kati yao.
Wanandoa Musila na Angel

Msanii wa injili Guardian Angel na mpenziwe Esther Musila wamesherehekea miaka miwili tangu wafunge ndoa yao rasmi.

Musila kupitia ukurasa wake wa Instagram alishiriki msururu wa picha nzuri wakiwa pamoja na kusisitiza kwamba Angel ndiye mwanamume bora ambaye amemfaa kwa kila kitu katika kipindi cha miaka miwili pamoja.

Musila alisema kwamba katika hadithi za kimapenzi ambazo zitasimuliwa, bila shaka yao itajitokeza mbele kama hadithi bora, huku akisema kwamba msanii huyo alibadilisha kabisa mtazamo wake katika mduara wa mapenzi.

“Siku hii miaka miwili iliyopita, nilifunga ndoa na rafiki yangu mkubwa na kati ya hadithi zote za mapenzi ulimwenguni, hadithi yetu itakuwa ninaipenda zaidi. Hii imekuwa safari nzuri, na mimi bado ni bibi arusi wako, na wewe bado ni bwana harusi wangu. Bado ni honeymoon...” alisema Musila.

“Tukitafakari juu ya safari yetu, kuna mambo 3 ambayo yatadumu daima; IMANI, UPENDO, na TUMAINI. Kubwa kwetu ni UPENDO. MAPENZI YAMESHINDA!! Kila siku, ninakupenda zaidi kuliko siku iliyopita. Unawafanya Mr & Bibi waonekane rahisi sana....” aliongeza.

“Mume wangu mpendwa, ulifafanua upya maana nzima ya uandamani. Bado nashangaa jinsi unavyokaa vizuri katika ndoa yetu. Asante kwa kuwa chanzo cha daima cha furaha na nguvu. Heri ya kumbukumbu ya miaka kwetu! Nakupenda G ❤️❤️❤️.”

Wawili hao walipatana miaka michache iliyopita katika hafla moja na mapenzi yao yakaanza hapo hadi pale walipofunga ndoa ya faragha Janauri mwaka 2022.

Musila licha ya kupokea kashfa kutoka kila kona kwa kukubali kuingia katika mapenzi na mwanamume ambaye yeye [Musila] anamshinda kwa takribani miaka 20, bado hajawahi aibika kushiriki hadithi ya mapenzi yao hadharani.

Ama kwa kweli, mwisho wa siku mapenzi ndio hushinda!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved