logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Andrew Kibe ndiye 'role model' wangu, nikimpata nampa hug kama dakika 10 - Brian Chira

“Yule jamaa ni gwiji wa kukuza maudhui, anaelewa maudhui ni nini," Kibe alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 January 2024 - 13:58

Muhtasari


  • • Chira alimtaja Kibe kama mtu ambaye anampa msukumo kwa jinsi anavyofanya kazi yake.
Mwanatiktoker Brian Chira amtamani Kibe kimapenzi.

TikToker Brian Chira kwa mara nyingine tena ameelezea upendo wake kwa mkuza maudhui Andrew Kibe.

 Chira ambaye si mara ya kwanza kuelezea jinsi anavyomkubali na kumpenda Kibe alisema kwamba hivi karibuni ataanzisha podkasti yake katika mtandao wa YouTube na vitu vingi atakuwa anaviiga kutoka kwa Andrew Kibe.

Chira alimtaja Kibe kama mtu ambaye anampa msukumo kwa jinsi anavyofanya kazi yake na kusema kwamba ikaja kutokea siku wamekutana, atamkumbatia kwa hadi dakika kumi hivi bila kumuachilia.

“Andrew Kibe ndiye role model wangu muda wote. Ninampenda Andrew Kibe, aki mimi sijui nisemeje, nikimpata tu mimi namkumbatia kama dakika 10 hivi,” Chira alisema.

Akiulizwa sababu ya kumtaja Kibe kama mtu ambaye angependa kufuata nyayo na nyendo zake katika kukuza maudhui, Chira alisema kwamba anamkubali na kumheshimu kwa jinsi anavyofanya kazi yake, licha ya kupata pigo kwa kufungiwa chaneli yake ya YouTube mwaka jana.

“Yule jamaa ni gwiji wa kukuza maudhui, anaelewa maudhui ni nini na anayasema vivyo hivyo jinsi yalivyo bila kuficha. Sio yule mtu wa kupiga piga kona eti kisa naogopa sitapata kukubaliwa na corporate, ama kisa kuogopa kwamba kampuni Fulani zitafanya kazi na wewe au la. Hiyo ndio sababu ninamkubali, huwa hafichi, anatoboa wazi bila woga. Na hicho ndicho ninataka kufanya na chaneli yangu ya YouTube,” Chira alisema.

Takribani miezi 10 iliyopita, Chira alifanya video kwenye TikTok akikiri mapenzi yake kwa KIbe na kusema kwamba alikuwa anavutiwa na ndevu zake.

Chira alisema kwamba ameshindwa kujizuia kila mara anapoona ndevu za mwanablogu Kibe na kumtaka kumtafuta angalau kwa busu.

“Andrew Kibe haki nakutafuta sababu hizo ndevu zako… Mungu wangu, mimi nakutaka Kibe nakutaka wewe. Hebu njoo nibusu hii midomo yangu…” Chira alisema katika video hiyo.

Ila safari hii anaonekana kuvutiwa Zaidi ya utendaji kazi wa Kibe katika kutafuta na kukuza maudhui.

Kwa bahati mbaya, akaunti ya Kibe ya YouTube ilifutwa mwaka jana kutokana na kile kilisemekana kwamba ni mwendelezo wa kuwashambulia na kuwadhalilisha wanawake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved