Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtoto wa kiume na binti wa kambo wa mwigizaji maarufu wa vichekesho wa Nigeria John Okafor, maarufu Mr Ibu, kutokana na madai kuwa waliiba pesa zilizokusudiwa kwa matibabu ya mwigizaji huyo.
Onyeabuchi Okafo na Jasmine Okekeagwu wanadaiwa "kumiliki simu ya mwigizaji huyo na kuingilia maelezo ya benki", kabla ya kuiba Naira milioni 55 ($60,700; £47,800).
Pesa hizo ni sehemu ya fedha ambazo zilikuwa zimechangwa na mashabiki na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya matibabu ya mwigizaji huyo, baada ya kuugua kwa muda mrefu mwaka jana.
Ugonjwa huo ulisababisha kukatwa kwa mguu mmoja wa Okafor.
Nyota huyo wa Nollywood pia alifanyiwa upasuaji mara tano, familia yake ilisema.
Mamlaka imepata naira 50m, vyombo vya habari vya ndani vinasema, vikimnukuu msemaji wa idara ya upelelezi wa jinai ya polisi, Mayegun Aminat.
Washukiwa hao wawili walikuwa wakipanga kutorokea Uingereza, kulingana na Bi Aminat.
Mahakama ya Lagos imewaachilia wawili hao kwa dhamana ya Naira 15m huku uchunguzi ukiendelea, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi Mach