Mbunge wa Keiyo Kusini, Bw Gideon Kimaiyo mnamo siku ya Jumatano alichapisha tena video ya mtandaoni ya mwimbaji Millicent Jepkorir almaarufu Marakwet Daughter akimsihi amfanye mke wake.
Katika video hiyo ambayo imekuwa ikisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, mwimbaji huyo wa kibao ‘Mali Safi Chito’ alisikika akijipeana kwa mwanasiasa huyo huku akibainisha kuwa yuko tayari kuolewa naye.
Mwimbaji huyo alimtaka Bw Kimaiyo kupiga hatua akitangaza kwamba anasubiri amtoe sokoni.
"Kuja unitoe soko, Mbunge wa Keiyo Kusini, Gideon Kimaiyo, nakusubiri babe," Marakwet Daughter alisikika akisema.
Alibainisha kuwa mbunge huyo wa muhula wa kwanza hana mke kwani bado anamsubiri.
“Wee, ndiye huyu mimi. Kuja nikupige busu. Babe, kuja nataka niende bungeni na wewe,” alisema.
Binti wa Marakwet hata hivyo alibadilisha kauli hiyo mara moja na kueleza kuwa yuko tayari kutuli nyumbani, kafanya ukulima wa mimea na wanyama huku mbunge huyo akiendelea na kazi yake jijini Nairobi.
Hata hivyo, alimuonya mwanasiasa huyo dhidi ya kutafuta wasichana wengine jijini Nairobi iwapo wataoana, akisema kwamba atakuwa amemngoja nyumbani kila mara.
“Njoo baby njoo, ukikataa nitakujia. Si ushaniona,” alisema
Wakati akijibu ombi la mwimbaji huyo kupitia mtandao wa kijamii wa X, mbunge huyo wa Keiyo Kusini alisema, "Haiya hii imeenda."
Makumi ya watumiaji wa mtandao wametoa hisia mseto kuhusu majibu ya Bw Kimaiyo.
Sereti Tonkei aliandika, “Mhesh tuite harusi bana.”
Mbunge akajibu, “Anivutie kwanza.”
Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao wengine;-
Saleem: Mhesh wanajileta tu.
Boniface G. Mwangiu: Wah! Saidia vile unasaidia pale kwa mashule. Toa yeye soko.
Daniel Lairuka Sindani: Fanya kitendo sharp, usiache hii opportunity ikupite.
Steph’ Gunte: Mhesh usiwache Mali safi kama hiyo. Bara hizi hazikuji mara nyingi.