Seneta mashuhuri wa kuteuliwa Karen Njeri Nyamu alijibu kwa kejeli baada ya shabiki mmoja kumkejeli kwa madai ya kuzaa na mume wa mtu mwingine.
Mwanasiasa huyo aliyezingirwa na utata mwingi alikuwa amechapisha picha nzuri ya mtoto wake wa pili, Samuel Muchoki Jr, wakati mwanamitandao alipomshambulia kwa kuzaa watoto wawili na mwimbaji Samidoh.
“Karenzo unakuaga mrembo lakini sasa na huo urembo wote na figure, find your own omuhubby issa problem why?” Syljayee Jumah alimwandikia seneta Nyamu kwenye mtandao wa Facebook.
Aliongeza, “Ulipata wapi nguvu ya kuzaa na mume wa watoto wawili.. Once bitten twice shy.”
Katika majibu yake, Bi Nyamu alishangaa ni kwa nini mwanamtandao huyo alionekana kushangazwa huku akidokeza kuwa bado hajamaliza kuzaa na mwimbaji huyo wa Mugithi.
“Ati 2 kids ni kama nimemaliza kuzaa na yeye,” Karen Nyamu alijibu na kuambatanisha kauli yake na emoji za kucheka.
Seneta Karen Nyamu ni mama wa watoto watatu, watoto wawili wa kike na mmoja wa kiume. Alipata binti yake mzaliwa wa kwanza na mpenzi wake wa zamani DJ Saint Kelvin huku watoto wake wengine wawili wakitokana na uhusiano wake wa sasa na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.
Takbriban miezi mitatu iliyopita, Karen Nyamu na Samidoh walimsherehekea mtoto wao wa kwanza pamoja katika siku yake maalum.
Samuel Muchoki Jr, ambaye ni mtoto wa pili wa seneta huyo, aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mwezi Novemba na wazazi wake walichukua fursa hiyo kueleza upendo wao kwake.
Katika ujumbe wake kwa mvulana huyo mdogo, seneta Nyamu alizungumzia jinsi anavyojivunia yeye na kuahidi kumuunga mkono kila mara.
“Siku zote nitakushangilia kwa sauti kubwa mwanangu. Hutawahi kuwa na shaka kuhusu shabiki wako mkubwa ni nani,” Karen Nyamu aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Aliambatanisha ujumbe wake na video ya mvulana huyo akicheza densi ndani ya hoteli huku wimbo wa Samidoh na Joyce Wa Mamaa ‘Wendo wi Cama’ ukichezwa.
"Heri ya kuzaliwa ya miaka mitatu Tami Tami. Prince of good vibes, "aliandika.
Kwa upande wake, Samidoh alisherehekea ukuaji wa haraka wa mtoto huyo wake na kumtakia baraka zaidi maishani.
"Wakati unaenda na unakua kuwa mtu mdogo wa kushangaza. Kila tabasamu, Kila hatua muhimu ni hazina. Hapa kwa vicheko zaidi, upendo, na matukio mengi. Heri ya siku ya kuzaliwa mwanangu,” aliandika Samidoh