Mwanamuziki anayejulikana kama Stivo simple boy alijulisha mashabiki wake katika mtandao wa kijamii kuwa video vixen wake Stafriza Adema, ameaga dunia.
''Nilifanya kwa Roho yangu yote ku support msani JUMA BOY na wewe pia ulikubali kuskia wito ukakuja ukakuwa VIXEN kwa ngoma yetu... week Moja Sahi after video shoot naskia umekufa hauko Tena na Mimi 🥹🥹🥹 hii imenivunja sana moyo ..siko sawa sitakuona Tena .nilikosea wapi Mungu wangu 🥹🥹🥹@star_adema REST IN PEACE mama @didykimeu tutoe tu ngoma no option...@jumaboy_j.b ðŸ˜ðŸ˜”😔", Stevo aliandika kwa Instagram.
Msichana huyo alishirikishwa kwenye wimbo wa Simple Boy na Jumaboy ambao unaitwa sherehe yenye imetokea leo.
Inasemaka kuwa Adema alikutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha. Alikuwa mtandaoni mara ya mwisho saa tano siku alipoaga dunia.
Inadaiwa kwamba wenzake walitoka kwenye klabu ya usiku saa tano na na kugundua mwili wake ukiwa umelala pale ikabidi waende wajulishe maafisa wa polisi
Adema alikuwa mwanafunzi wa chuo cha KMTC na alikuwa na ndoto za kuwa mwanamitindo na video vixen.
Sababu ya kifo chake cha ghafla bado haijafahamika na uchunguzi wa maiti utafanywa ili kubaini kilichotokea.