logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Manzi wa Kibera: Kwa nini napenda kugawa penzi kwa wazee kuliko kwa kina Kevo na Brayo

Alisema kwamba ikiwezekana atafunga harusi na wote wawili,

image
na Radio Jambo

Yanayojiri29 February 2024 - 04:18

Muhtasari


• Aliwashauri wasichana kuchagua kutoka kimapenzi na wazee kuliko kina Brayo na Kevo kama kweli wanataka kupunja maisha katika mstari wa kwanza.

Manzi wa Kibera na mpenzi mpya.

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera amefichua sababu kuu ya kupenda kuchumbiana na wanaume wazee kiumri kumliko.

Akizungumza na Kenya Online Media, Mrembo huyo kutoka Kibera alisema kwamba wazee ndio mpango mzima kwani wamejipanga na kujiweka sawa kuliko vijana wa kisasa – kina Kevo na Brayo.

Aliwashauri wasichana kuchagua kutoka kimapenzi na wazee kuliko kina Brayo na Kevo kama kweli wanataka kupunja maisha katika mstari wa kwanza.

“Mimi kitu naweza ambia wasichana wadogo ni kwamba, wazee ndio njia pekee ya kwenda. Kama unataka kina Kevo na Brayo, utalia kushinda huyo mtoto Kevo amekuzalisha. Lakini ukiwa na mzee, kila kitu kinajipa, hakuna za kukuhadaa. Anakuambia babe, unataka nini, shamba? Twende ushagoo nikuchukulie shamba,” Wambo alishauri.

“Lakini kina Kevo kila muda wanafikiria tu bend-over. Tafakari mimi vile niko mrembo hivi mtu anakuja kuniambia eti bend-over wakati kuna mzee mahali anatakakuniambia twende tuketi chini tukunywe. Mzee ananiambia twende tukunywe supu Village Market, shilingi 600 kwa kikombe,” aliongeza.

Mrembo huyo ambaye hivi majuzi amedai kurudiana na mzee wake wa awali, Nzioki mwenye umri wa miaka 67 alisema bado hajaachana na ‘new-catch’ Daniel Njau mwenye umri wa miaka 75.

Alisema kwamba ikiwezekana atafunga harusi na wote wawili, lakini akafichua kwamba wote hawajawahi kutana hata kama anaweka maisha yake wazi katika mitandao ya kijamii.

Manzi wa Kibera alisema kwamba wote hakuna anayeweza kufikia mitandao kwani alichukua simu zao zote na yeye ndiye huwaendesha jinsi anavyotaka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved