John Cena alionekana akiwa nusu uchi wakati akiwasilisha Tuzo la Academy kwa ubunifu wa mavazi bora, akitania katika maadhimisho ya miaka 50 ya mwanamume aliyetamba kwenye Tuzo za Oscar.
Muigizaji na mwanamieleka huyo alipanda jukwaani Jumapili usiku akiwa na bahasha iliyowekwa kimkakati ya tuzo ili kufunika sehemu yake ya siri, jambo lililoibua vicheko na makofi kutoka kwa watazamaji.
"Mavazi - ni muhimu sana," Cena alisema. "Labda kuna jambo muhimu zaidi."
Kisha akagundua kuwa hangeweza kufungua bahasha bila kuonyesha zaidi ya alivyotaka, na muandalizi wa Oscars Jimmy Kimmel aliamua kumsaidia.
Wagombea walipotangazwa, Cena alifanyiwa mabadiliko ya haraka ya mavazi yaliyoonekana kama vazi la toga lililotengenezwa kwa pazia. Kisha akatangaza mshindi wa Oscar.