Mwanzilishi wa kanisa la New Life Prayer Centre mhubiri Ezekiel Odero ameelezea hofu kuhusiana na vifo vya mapema vya vijana wengi nchini Kenya.
Kulingana na mchungaji Ezekiel, vifo hivi sio vya kawaida na na kuvihusisha na utoaji kafara.
Alisema kwamba vijana wadogo wananaswa bila kujua katika mtandao wa giza, ambapo maisha yao hutumiwa kama matoleo.
"Unaona vifo hivi vinavyowapata vijana wa kiume, vinahusishwa na viapo na mila. Jinsi wanavyojiua ni kuhusu hili. Mimi huwa nawaambia kuwa mtandao ni kitu kizuri, lakini ni kikubwa kuliko ulimwengu huu. Chagua mahali pa kuishi kwenye mtandao kwa sababu huwezi kuishi kila mahali kwenye mtandao."
Katika ombi lake Mchungaji Ezekiel aliwahimiza vijana kumgeukia Mungu na kutafuta kimbilio katika ufalme wake.
Alionya dhidi ya kuvutia kwa mtandao, akisema kuwa inaenea zaidi ya ulimwengu wetu wa kimwili.
"Vijana, mgeukieni Mungu. Nje ni mbaya. Vifo hivi vingi vinapaswa kutupa changamoto ya kumrudia Mungu. Hatuwezi kufa tu hivyo. Watu wanawatolea wengine dhabihu kwa madhabahu wanayotumikia. Ni dhabihu tu. Sio vifo vya kawaida. Wanaambiwa watoe dhabihu watu wanaowapenda zaidi. Na kwa sababu ya nguvu mbaya, kesi zao kawaida huisha bila haki", alisema mchungaji Ezekiel.