logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nikita Kering alazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa na ngo'mbe aliyekuwa akimkamua

Ng’ombe alimtupia teke kabla ya kusambaratisha shughuli nzima na kutupa ndoo kando

image
na Davis Ojiambo

Burudani30 March 2024 - 09:22

Muhtasari


  • • Akinukuu video hiyo, Nikita Kering alisema kwamba ilikuwa kuonyesha matukio ya sikukuu ya pasaka kwa ujumla.
  • • Msururu wa video hiyo kwenye ukurasa wake ulionyesha matukio mengine ya jinsi sikukuu yake ya pasaka ilivyoanza.
NIKITA KERING

Msanii Nikita Kering ameripotiwa kulazwa hospitalini baada ua kile kilichotajwa kama kujeruhiwa na ng’ombe aliyekuwa akimkamua shambani.

Katika klipu ambayo inaenezwa mitandaoni, msanii huyo mshindi wa tuzo alionekana akiwa amelazwa hospitalini baada ya awali kupakia klipu kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anamkamua ng’ombe shambani.

Katika video hiyo akiwa anakamua ng’ombe, Nikita alikuwa amevalia buti, jeans huku akiwa ameinaka kwenye maziwa ya ng’ombe akikamua huku akitabasamia kamera.

Akinukuu video hiyo, Nikita Kering alisema kwamba ilikuwa kuonyesha matukio ya sikukuu ya pasaka kwa ujumla.

Msururu wa video hiyo kwenye ukurasa wake ulionyesha matukio mengine ya jinsi sikukuu yake ya pasaka ilivyoanza, yakiwemo kuonekana jikoni akisonga ugali, akiandaa ‘mursik’ kabla ya tukio la kukamua ambalo lilimuendea mrama.

Ng’ombe alimtupia teke kabla ya kusambaratisha shughuli nzima na kutupa ndoo kando, huku Kering akionekana kupatwa japo kwa kiduchu na teke la ng’ombe na baadae kuonekana akiwa hospitalini na bendeji kwenye mguu wake wa kushoto.

Video hiyo ilipata hisia nyingi kutoka kwa watumiaji wa mtandao, wengine wakimuhurumia na wengine wakitaka kujua kwa nini alikuwa akikamua ng'ombe kwanza.

Tazama video hiyo jinsi sikukuu ya pasaka ilivyoanza vibaya kwa msanii huyo kutoka bonde la Ufa;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved