logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nimechoka, nimetoka kwenye tiktok, siwezi kuendelea!" Akothee atangaza, afichua sababu

Hii ni baada ya video iliyokejeli maendeleo yake kutengenezwa kwenye mtandao huo wa kijamii.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani06 April 2024 - 06:43

Muhtasari


  • •Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee mnamo Jumamosi asubuhi alitania kuhusu kufuta akaunti yake ya tiktok.
  • •Mwimbaji huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa tangazo hilo , akidai hawezi kuendelea.

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee mnamo Jumamosi asubuhi alitania kuhusu kufuta akaunti yake ya tiktok.

Hii ni baada ya video iliyokejeli maendeleo yake kutengenezwa kwenye mtandao huo wa kijamii ambao amekuwa akitumia kutangamana na mashabiki wake.

Mwimbaji huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa tangazo hilo , akidai hawezi kuendelea.

"Nimechoka, mweusi ilikuwa lazima? Nimeondoka kwenye tiktok rasmi, nimefuta akaunti yangu, siwezi kuendelea,” Akothee aliandika, na kuambatanisha taarifa hiyo na emoji za kucheka, kudokeza kwamba alikuwa anatania tu kuhusu kuondoka.

Pia alishiriki video hiyo iliyozungumza kuhusu yeye kuwa mweusi na aliyefilisika katika siku za nyuma.

“Esther was once black and broke. But when Esther see money, Establish...” mtangazaji kwenye video hiyo alisikika akisema.

Uchunguzi wetu hata hivyo umebainisha kuwa mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 bado yuko kwenye mtandao wa kijamii kufikia wakati wa kuchapisha habari hii.

Katika siku za nyuma, Akothee aliwahi kushiriki mtazamo wake kuhusu TikTok ambapo alielezea sababu yake awali kusita kujiunga na jukwaa hilo kwa sababu ya tabia yake ya kuchukua muda na kuenea kwa kelele na migogoro.

Katika maelezo ya safari yake kwenye mtandao huo wa kijamii, alidai kuwa awali alikuwa amepoteza akaunti tatu zenye wafuasi zaidi ya 100k kutokana na changamoto za usimamizi wa jukwaa hilo.

Mwimbaji huyo alisema licha ya changamoto hizo, meneja wake Nellyoaks, alimtia moyo kukumbatia Tiktok kwa sababu ya ufuasi wake mkubwa kwenye jukwaa hilo.

Alidai kuwa akaunti yake na ya meneja wake ziliripotiwa na hatimaye kusimamishwa, akihusisha vitendo hivyo na wivu na watu kutojiamini.

"Sijui kama nilipaswa kuomba ruhusa ya kujiunga na maisha yangu na simu yangu na mashabiki wangu au? Je, huu ni utani mkubwa?

Kwani nani anamiliki mtandao huu? Ama watu wako na hisa tujue tunanunue ngapi?” Akothee alisema muda fulani nyuma.

Aliongeza, “Wivu ukawa hauwezi kudhibitika, watu walinitumia video nikionywa nisijiunge na TikTok na kwamba nishikamane na Facebook na Instagram.

Kwa taarifa yako tu, akaunti yangu na na akaunti ya Nelly Oaks ziliripotiwa na kusimamishwa. Hivyo ndivyo wivu mbaya na ukosefu wa kujiamini unavyoweza kwenda."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved