logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sijawahi kuachwa na mwanamke yeyote- Diamond ajigamba

Diamond alikiri anapohisi kukosa nafasi, anafanya makusudi kwa njia ya kuumiza ili kumchokoza mpenzi wake kuondoka.

image
na Samuel Maina

Burudani04 May 2024 - 11:01

Muhtasari


  • •Diamond amefunguka kuhusu jambo la kustaajabisha huku akidai kuwa hajawahi kuachwa na mpenzi wake yeyote wa zamani.
  • •Diamond alieleza mbinu ya kipekee ya kukomesha uhusiano, akikiri anapohisi kukosa nafasi, anafanya makusudi kwa njia ya kuumiza ili kumchokoza mpenzi wake kuondoka.

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz amefunguka kuhusu jambo la kustaajabisha huku akidai kuwa hajawahi kuachwa na mpenzi wake yeyote wa zamani.

Katika mahojiano ya hivi majuzi kwenye Wasafi Media, msanii huyo mahiri alieleza mbinu yake ya kipekee ya kukomesha uhusiano, akikiri kwamba anapohisi kukosa nafasi, anafanya makusudi kwa njia ya kuumiza ili kumchokoza mpenzi wake kuondoka.

“Sijawahi kuachwa na mwanamke yeyote. Ninapochumbiana na nahisi kama mwanamke ananiingilia, ninafanya utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo yatamuumiza hadi anaachana na uhusiano huo,” alikiri waziwazi.

Licha ya historia yake ya kuwa na uhusiano wa hali ya juu na kuzaa watoto wanne, Diamond alishikilia kuwa wapenzi wake wote wa zamani wamekuwa na hisia kali zaidi kwake kuliko yeye.

Lakini je, kauli yake ni kweli ikichunguzwa?

Ndio, ni kweli ikiwa mtu ataangalia ushahidi ambao waangalizi wengi waangalifu wanaweza kujua kuhusu mahusiano yaliyotangazwa sana ambayo mwimbaji amekuwa nao kwa miaka mingi.

 Zari Hassan, mzazi mwenza wa kwanza wa Diamond alimuacha mnamo Februari 14, 2018 katika chapisho la kushangaza kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kumshutumu kuwa na mahusiano meingi.

Na sio yeye pekee! Mama mtoto wa tatu wa Diamond, Tanasha Donna pia alimwacha mwimbaji huyo baada ya kurudiana kwa muda mfupi mapema 2020 na pia alimshutumu mwimbaji huyo kwa kuenda nje ya mahusiano sana.

Isitoshe! Mwimbaji huyo ambaye hivi majuzi alikuwa akichumbiana na mpenzi wake Zuchu pia aliachwa naye wiki hii iliyopita.

Haya yanajiri baada ya hali nyingi za aibu ambazo mwanamuziki huyo alimuweka nazo hali iliyowafanya mashabiki wengi wa Zuchu kumtaka aachane naye.

Shida ya mwisho ilikuwa pale msanii huyo  alipotambulisha hadharani na kumkumbatia mmoja wa wapenzi wake wa kwanza moja kwa moja kwenye jukwaa wikendi iliyopita.

Lakini atabadilisha tabia yake na wapenzi wanaofuata? Ni yeye pekee anayejua.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved