Zari Hassan ametoa heshima kwa aliyekuwa mume wake na marehemu mfanyabiashara Ivan Semwanga. Yeye na Ivan walizaa wana watatu kabla ya kifo chake.
Alifariki akiwa na umri wa miaka 39 tarehe 25 Mei 2017 alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Steve Biko Academic, Pretoria, Afrika Kusini.
Katika ujumbe wake wa Instagram, Zari aliweka picha ya Semwanga, wana wao watatu na yeye mwenyewe na kuandika ujumbe wa kumheshimu, huku akimuhakikishia kwamba watampenda milele na daima.
"Miaka saba inaonekana kama jana. Mwenyezi Mungu aendelee kukupumzisha kwa amani. Tutakupenda daima." Zari aliandika baada ya ku[pakia picha hiyo mitandaoni.
Wakati huo Zari alikuwa na jukumu la kutangaza kifo cha Ivan, jambo ambalo alilifanya kwenye mtandao wake wa kijamii.
"Mungu anawapenda wale ambao ni maalum na hivyo ndivyo ulivyokuwa na nadhani ndiyo sababu alitaka wewe mwenyewe. Umegusa na kusaidia maelfu, ulifanya maajabu nakumbuka uliniambia “life is too short Zee let me live it to the fullest”, saa hii ya giza sana inaeleweka kwanini uliniambia maneno hayo kila mara. Kwa wana wako, ulikuwa shujaa-aina fulani ya superman. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa mbele yako anajua jinsi ulivyokuwa mtu wa kupendeza. Utakumbukwa na kukumbukwa kwa njia nyingi sana. Ulikuwa IVAN MKUU!” Aliandika.