Mwanamke mmoja amevunja ukimya kwa kusimulia kisa kilichompelekea kufutwa kazi baada ya saa 3 tu katika kazi yake mpya.
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanamke huyo alionyesha mshtuko baada ya mkurugenzi wake kumfukuza kazi baada ya saa 3 tu katika jukumu lake jipya.
Wengi walikuwa wameenda kwenye sehemu ya maoni walielezea maoni tofauti kuhusu hili, wengine wakimshauri kumchukulia hatua za kisheria mwajiri wake, na mwanamke huyo sasa ameingia kwenye mitandao ya kijamii kuvunja ukimya wake na kuelezea ukweli wa mambo.
Mwanamke huyo alifichua kuwa NYSC ilikuwa imemtuma kwa kampuni ambapo alikubaliwa na alikuwa ameidhinishwa katika stakabadhi zake zote.
Alisema kwamba alikuwa ameanza tena wiki ya kwanza ya Juni, kama vile alivyoagizwa kufanya.
Hata hivyo, alipokuwa akifanya kazi kwenye dawati lake, mwanamke aliyekuwa amemhoji alimweleza kwamba MD alitaka kumuona.
Alisimulia majibizano ya maneno yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba hicho, na jinsi MD alivyomfukuza kazi kwa sababu shahada aliyokuwa nayo haikuwa ile waliyoihitaji katika shirika, licha ya kwamba bibi huyo alionyesha kwamba ana ujuzi unaohitajika katika idara waliyo mwajiri.
“Kwa muktadha, nilitumwa pale na NYS mwezi jana nikawapa CV yangu, nikafanya usahili wa kuomba kazi na nikafanikiwa na nikapatiwa barua ya kukubaliwa kuingia kazi. Wiki tatu baadae nikaingia kazini – waliniambia niingie mwezi Juni na hicho ndicho nilifanya.”
“Nilifaa kuingia 8am lakini mimi nilifika 7am kwa sababu nilikuwa na hamu ya kufanya kazi. Mwanamke aliyenihoji mwezi uliopita alikuja na kunipeleka kwenye dawati nitakalokuwa nikifanyia kazi, akanitambulisha kwa wafanyikazi wenzangu na kunipa majukumu ya kufanya.”
“Kila kitu kilikuwa sawa na kisha mwanamke yule akaja na kuniambia kwamba MD wa kampuni anahitaji kuonana na mimi. Nilienda kwa ofisi ya MD akaniuliza taaluma niliyosomea nikamwambia ‘Sociology’ na alionekana kughadhabika ghafla akisema alishaonya dhidi ya kuajiriwa kwa watu wenye digrii hii katika kampuni yake.”
“Niliondoka nikarudi kwa dawati langu lakini nilitatizika kiakili nikijiuliza mbona wananifanyia hivi wakati walikuwa na wiki 3 za kunikataza nisije kazini. Nikaendelea kufanya kazi na saa chache baadae yule mwanamke akaja na kuniomba radhi akiniambia kwamba imebidi waniachilie niondoke na kuomba msamaha kwa kunipotezea muda wangu….”
Mtazame hapa chini akiongea...