TikToker Kelvin Kinuthia anazidi kuwapa ushindani wa kipekee kina dada katika suala zima la urembo.
Kinuthia, ambaye ni mwanamitindo wa mavazi ya kike licha ya kuwa wa kiume amekuwa akijishaua na kujionyesha jinsi alivyo hodari katika ladha yake kwenye fasheni ya kike.
Ili kujiboresha na kuvutia mwonekano wa kisichana Zaidi, Kinuthia sasa ametangaza kwamba ameanza mchakato wa kuondoa ndevu zake ili kutupilia mbali kabisa kiashiria chochote cha kumtoa kama wa jinsia ya kiume.
Kupitia insta story yake, Kinuthia alitangaza kwamba ameanza mchakato huo huku akithibitisha kwamba amekuwa akiteseka sana kujaribu kujionesha kama mwanamke lakini ndevu mara nyingi humuanika na kumsaliti.
“Guys niko na furaha kubwa kuwataarifu kwamba hatimaye nimeanza mchakato wa kuondoa nywele maarufu kama ‘laser hair removal’. Kusema kweli nimeteseka sana na ndevu zangu, niko na furaha sana sasa,” Kinuthia aliandika.
Akiitaja kama safari mpya, Kinuthia aliwaomba mashabiki wake kujiunga na yeye katika safari hiyo ya kipekee kushuhudia jinsi atatokomeza ndevu zake na hivyo rasmi kuufanya uso wake kuwa kama wa kike bila kiashiria chochote cha jinsia ya kiume.