Mwanzilishi wa kanisa la Neno Evangelism Center James Ng’ang’a ambaye anapenda kujiita ‘Kamanda’ ameeleza ni kwa nini alishindwa kujitokeza kwenye maandamano ya barabarani, hata baada ya kuahidi kujitokeza.
Mchungaji Ng’ang’a ambaye alikuwa akizungumza wakati wa ibada ya kanisani, alisema sababu ni kwa sababu aliambiwa kuwa yeye si Gen Z.
“Ilikua niende maandamano vijana wakasema hiyo ni maandamano ya G. Wakasema mimi ni Z ngapi? kuna group tatu wakasema we mzee we ni wa sijui ni G gani iko hapa…niliambiwa mimi sio G N.” Mchungaji Ng’ang’a alisema.
Mchungaji huyo alionekana kuhangaika kueleza hoja yake, alichomaanisha ni kwamba aliambiwa asiende kwa sababu yeye ni mzee na si Gen Z, na hivyo akaamua kukataa kushiriki maandamano.
Mwazilishi huyo wa kanisa ya Neno Evangelist Mchungaji Ng’ang’a alikuwa amehakikishia umma kwamba angeungana nao katika maandamano wiki iliyopita siku ya Jumanne.
"Hata mimi nitakuwa kwa hiyo maandamano sasa mje na teargas mnipige,ninaweza zungumza kama mwananachi nitaacha pastor hapa wacha mtaniona tuh." Mchungaji Ng’ang’a alisema.
Mchungaji Ng’ang’a alishiriki masikitiko yake na Serikali ya Kenya Kwanza kwa kulenga ardhi yake kila mara, ambayo anadai haifai kupokonywa kutoka kwake.
Mchungaji Ng’ang’a amekuwa akitofautiana na Serikali ya Kenya Kwanza akisema hapendi jinsi inavyowatendea watu wake.