logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond ajawa na furaha baada ya Jason Derulo kufanya challenge ya Wimbo wake, Komasava

Diamond alikiri kuwa na furaha isiyomithilika kuona wasanii wakubwa wakivutiwa na utunzi wake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 July 2024 - 07:35

Muhtasari


  • • Derulo alirekodi video akiwa na rafiki yake wakifanya challenge ya Komasava, jambo ambalo limemtoa 'Simba' pangoni.

Msanii wa Bongo Diamond Platnumz amedhihirisha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa ambayo Wimbo wake wa Kimasava unazidi kuvuta kapuni.

Baada ya kupaisha wimbo huo kwa katika mataifa mengi tu baronial Ulaya, haswa Ufaransa, safari hii wimbo huo umevuka mipaka na kuwavuta wasanii kutoka Marekani ya Kaskazini.

Msanii wa Kanada, Jason Derulo ni wa hivi punde kuvutiwa na wimbo huo na kushindwa kuzuia minenguo yake kwa midundo ya Komasava.

Derulo alirekodi video akiwa na rafiki yake wakifanya challenge ya Komasava, jambo ambalo limemtoa 'Simba' pangoni.

Diamond alikiri kuwa na furaha isiyomithilika kuona wasanii wakubwa wakivutiwa na utunzi wake.

"Kaka, huyo ni Jason Derulo kwenye challenge ya Komasava. Siwezi jieleza jinsi ambavyo ninahisi kwa furaha na shukrani niliyonayo kumuona akifanya challenge hii. ICON, GOAT, IDOL," Diamond alisema.

Akiusifia wimbo huo, Platnumz alisema kwamba midundo yake inaweza ikamfanya mtu kulazwa kwa mshtuko wa ghafla.

"Dah, huu wimbo wa Komasava unaweza ukafanya mtu hata akalazwa kwa klipu zake za kushtua ghafla."

Diamond aliachilia wimbo huo takribani miezi miwili ilyopita akiwashirikisha wasanii kutoka Afrika Kusini, Khalil Harrison na Chley.

Wimbo wenyewe ni wa mdundo wa Amapiano na tauari umemfanya akakutana na mchezaji nguli wa Ufaransa Paul Pogba ambaye walionekana wakiufurahia wakifuatilia mechi za Euro nchini Ujerumani wiki tatu zilizopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved