Msanii Diamond Platnumz amezugumza kwa mara ya kwanza kuhusu kifo cha Khadija Shaibu almaarufu Dida ambaye aliaga dunia mapema mwezi huu.
Kama mkurugenzi wa Wasafi media, Diamond alitarajiwa kuzungumza kuhusu kifo cha mtangazaji huyo ambaye alikuwa kama ndugu na rafiki yake, kitu ambacho hakufanya.
Kwa mahojiano, Diamond alikiri kuwa amekuwa akikwepa kuzungumzia lolote linalohusiana na Dida kwa kuwa ni msiba ambao una uzito mkubwa sana.
“Nafikiri nimekuwa nikiikwepa sana bila kuzungumzia au kugusia lolote linachohusiana na Dida. Hili ni kwa sababu ya uzito wa msiba huu ulionikuta. Kutokana na uzito wake, nafikiri sikua najihisi kama sijakuwa tayari kuzungumzia chochote kuhusinana na msiba huu. Ndio maana hata sijakuwa nazungumza rasmi sijasema chochote,”
Alisema kuwa atakapokuwa tayari kuzungumzia msiba huo atafunguka na kusema.
“Sidhani kama niko tayari sana kuzungumzia ndio maana nakwepa sijazungumza popote. Siku nikiwa tayari nitazungumza na kusema ,”
Diamond anasema kuwa Dida alipoaga dunia ni yeye alipigiwa simu wa kwanza kabla ya mtu yeyote kuambiwa.
Dida aliaga dunia
mapema mwezi huu akipokea matibabu hospitalini Dar es Salaam na
kuzikwa Jumamosi kulingana na mila ya Waislamu.
Alikuwa ameajiriwa kama mtangazaji kwenye kituo cha redio cha Wasafi FM kinachomilikiwa na msanii maarufu wa bongo Diamond Platnumz. Dida alijulikana kwa kufanya kipindi cha asubuhi kwa jina ‘MashamSham’ pamoja na Idris Wa Kitaa na Juma Lokole.
Umaarufu wa Dida ulijitokeza akifanya kazi katika kituo cha Times FM kipindi cha ‘Mitikisiko ya Pwani’